Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Pwani, Goodluck Charles
Wateja
wa Tigo katika mikoa ya Lindi na Mtwara hivi sasa wanaweza kufurahia
kuunganishwa na intaneti ya kasi kufuatia kampuni hiyo kupanua huduma
yake ya 4G LTE katika miji hiyo ya kusini mwa Tanzania. Teknolojia ya
4G LTE ni ya kasi takribani mara tano zaidi ya teknolojia ya 3G
iliyopo katika soko kwa hivi sasa.
Kwa
mujibu wa Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Pwani, Goodluck Charles upanuzi
huo unafuatia kuzinduliwa kwa mafanikio kwa huduma hiyo katika miji
mingine 14 nchini.
Charles
anasema “Kupatikana kwa teknoplojia ya 4G katika mikoa ya Lindi na
Mtwara kunaonesha kuwa Tigo kwa mara nyingine jinsi ilivyojikita katika
kuboresha mabadiliko katika mtindo wa maisha ya kidijitali na kuongoza
kwake katika kutoa teknolojia ya kisasa na ubunifu ndani ya soko.”
Huduma
ya 4G LTE inamaanisha kurambaza kwa kasi kubwa, kupakua vitu kutoka
katika intaneti na kufanya miito ya mawasiliano ya simu kwa kuonana
(skype). Hali kadhalika inawezesha wateja kwa kiwango kikubwa
kutiririsha video na hata mikutano ya video. Hali kadhalika na matumizi
mengi kama vile kufanya mkutano kwa video, ubora wa hali ya juu, blogu
za video michezo na kupakua video kutoka kwenye mitandao ya jamii.
Mtwara
na Lindi ni vituo muhimu vya biashara katika mikoa ya kusini mwa
Tanzania. “Tunataraji kwamba wakazi wa Lindi na Mtwara, wafanyabiashara
wanaojishughulisha na biashara ya korosho, uvuvi na wadau katika sekta
ya mafuta na gesi watafurahia uzoefu wa teknolojia ya 4G LTE na
kufanya shughuli za kijamii kwa njia ya mtandao kwa urahisi
zaidi,”anafahamisha.
Anaongeza
kusema, “Ninapenda kuwajulisha wateja wetu kwamba bei bei kwa ajili ya
vifuurushi vya intaneti ya 4G LTE ni sawa na ile ya vifurushi vya 3G,
na hali kadhalika wateja wote walio na kadi ya simu ya 4G LTE
watanufaika kwa kupata GB 10 bure watakapojiunga kwa mara ya kwanza na
mtandao wa 4G LTE. Hii inamaanisha kwamba mteja mwenye thamani
anahitaji kuwa na kifaa kinachowezessha teknolojia ya 4G LTE, ama kiwa
simu ya kisasa au kisambazio pamoja kadi ya simu. Wanaweza kubadilisha
au kupata kadi ya simu ya 4G kutoka katika maduka yetu ya Lindi na
Mtwara.”
Anaarifu
kuwa mipango ipo njiani kupanua huduma hiyo hadi kufikia mikoa
mitano iliyobakia na hivyo kuwa imesambazwa nchini kote ifikapo
mwishoni mwa mwezi huu wa Oktoba.
No comments:
Post a Comment