Thursday, November 17, 2016

MREMA AJITOKEZA KUJITETEA KWA RAIS MAGUFULI LEO,SOMA HILI ANALOLALAMIKIA

Mrema
Mwenyekiti wa Taifa wa Bodi ya Parole,Dk. Augustine Mrema akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani) , Jijini Dar es Salaam leo.

MWENYEKITI wa Taifa wa Bodi ya Parole, Dkt.  Augustine Mrema  amemwandikia barua Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kulalamikia jeshi la Magereza kukwamisha mpango wake wa kuwatoa wafungwa ambao tayari wameshalipiwa fedha na wasamaria wema baada ya kukidhi vigezo.

Dkt. Mrema ameyasema hayo mchana huu wakati wa kutoa taarifa yake hiyo kwa waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam kuzungumzia suala lake hilo la Maafisa wa Magereza kusitisha hatua ya kukatisha mpango wake licha ya kuwalipia wafungwa waliokidhi vigezo.


“Mimi nimeona nisinyamaze,napaza sauti nataka Rais aone, ajue kama magereza yetu yanashida na tunalotatizo kwa nini mpango huu umesimamishwa na umesitishwa tumekosea wapi?. Nimesha muandikia barua Waziri Mkuu kulalamikia jeshi la Magereza kukwamisha mpango huu na watu 43 tayari tumesha walipia faini hiyo lakini bado wapo magerezani wanasota. Mrema amefanya kosa lipi? Ama Mama Mchungaji Getrude Rwakatare amekosa nini? Mpaka wamesitisha zoezi hili” amesema Mrema kwa waandishi wa habari.

Hata hivyo Mtandao huu ulipohoji juu ya kama fedha zilizolipwa za Mchungaji Mama Rwakatare zinaweza kurejeshwa ama la!, Mrema amesema kuwa suala hilo lipo chini ya Mama Rwakatare mwenyewe ila wanasubiria hatua kutoka kwa Rais na Waziri Mkuu ambapo wameshatoa malalamiko yao juu ya suala hilo.
Dk Mrema amewaonyesha wandishi wa habari  nyaraka ikiwemo risiti mbalimbali walizofanya malipo kwa ajili ya kuwatoa wafungwa hao ambapo amesema haki ya kuzuia mpango huo imeweza kumuumiza vibaya kwani wasamaria wema walioweza kujitolea fedha za mpango huo imewagusa pia.

Pia ameongeza kuwa,  mpaka sasa magereza mbalimbali kuna msongamano wa wafungwa ambao wanahitaji msaada wa kutoka ila hawajapata fedha za kulipiwa hivyo pindi wasamalia wema kama Mchungaji Mama Rwakatare wanapojitokeza wanatakiwa kupongeza na wala si kupinda kona kona.

Hivi karibuni Jeshi la Magereza lilisitisha shughuli iliyokuwa ikiendeshwa na Mchungaji Getrude Lwakatare ya kuwalipia faini wafungwa walioko magerezani hadi hapo utaratibu mwingine utakapotolewa.


Awali ilidaiwa kuwa Mpango huo unaofanywa na Lwakatare kwa kushirikiana na Mwenyekiti wa Taifa wa Bodi ya Parole, Augustine Mrema tayari umewezesha wafungwa 78 kutoka magerezani baada ya kuwalipia faini inayofikia Sh25 milioni.
Kwa mujibu taarifa zilizonukuliwa katika moja ya vyombo vya habari hapa mchini vilieleza kuwa, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma, Antonio Kilumbi alisema amepata maelekezo ya kusitishwa kwa mpango huo kutoka ngazi ya juu ya jeshi hilo na  kuongeza kuwa, wananchi wengine bado wanaweza kuwalipia faini hiyo ndugu zao.

Hata hivyo Mrema amesema  mpango huo ulilenga kupunguza msongamano wa wafungwa magerezani na kuipunguzia Serikali gharama za kuwahudumia wafungwa hivyo usitishwaji huo unalenga  kurudisha nyuma juhudi za Bodi hiyo  katika kuwasaidia wafungwa waliokizi vigezo.

CREDIT --MWANGALA BLOG


No comments: