Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar Es salaam kwa
kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama limejipanga ipasavyo
kuhakikisha amani na utulivu vinatawala wakati
wa kuazimisha sikukuu ya uhuru itakayofanyika tarehe 09/12/2016 katika
uwanja wa uhuru jijini Dsm.
Sherehe hiyo itahudhuriwa na viongozi na wakuu wa
nchi za jirani, viongozi wa kitaifa, mabalozi, wanasiasa mbalimbali pamoja na
viongozi wengine waliolitumikia taifa na kustaafu.
Aidha tunaomba wananchi wasiwe na shaka yoyote ya
kiusalama na pia wajitokeze kwa wingi katika uwanja huo ili kusherehekea
sikukuu hiyo kwa utulivu na amani.
Kutakuwa na doria kuzunguka uwanja huo pamoja na
maeneo mbalimbali ya jiji ya jiji la Dar
Es salaam.
Sambamba
na hilo pia tarehe 12/12/2016
ni sikukuu ya MAULID, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limejipanga
vizuri katika kuhakikisha katika kipindi chote cha kuazimisha sikukuu hii
ulinzi na usalama unakwepo hususan katika maeneo ya misikiti ambapo ibada zitafanyika.
Kutakuwa na doria ya miguu, askari kanzu, askari
wa Mbwa na farasi, FFU na askari wa doria za magari ili kuhakikisha sikukuu
inasherekewa kwa furaha na amani.
Pia askari watafanya doria katika maeneo yote
yenye mikusanyiko mkubwa kama fukwe za bahari ya Hindi na maeneo mengine ya
starehe ili kuzuia vitendo vya uvunjifu wa amani.
Disko toto haziruhusiwi na wazazi/walezi
wasiwasiwaache watoto wao watange tange ovyo.
Nyumba zisiachwe bila mwangalizi kwa kipindi cha
sherehe kwani wahalifu wanaweza kutumia mwanya huo kufanya uhalifu.
POLISI KANDA MAALUM DSM WAKUSANYA TSH 451,590, OOO /=
KUPITIA TOZO ZA MAKOSA YA USALAMA BARABARANI
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dsm kupitia kikosi
chake cha usalama barabarani kimekamata makosa mbalimbali ya usalama barabarani
kwa kipindi cha kuanzia tarehe 02/12/2016 hadi tarehe 07/12/2016 na kuingizia
serikali mapato ya ndani kama ifuatavyo;
1.
Idadi ya
magari yaliyokamatwa - 13,496
2.
Idadi ya
Pikipiki zilizokamatwa - 1,296
3.
Daladala
zilizokamatwa
- 5,713
4.
Magari
mengine (binafsi na malori) - 7,783
5.
Bodaboda
waliofikishwa Mahakamani
kwa makosa ya kutovaa helmet na
kupakia mishkaki - 4
6.
Jumla ya
Makosa yaliyokamatwa - 15,053
Jumla ya Fedha za Tozo zilizopatikana TSH 451,590,OOO/=
Aidha madereva
wanatakiwa kuwa makini katika kipindi hiki cha kuelekea mwisho wa mwaka ili
kuepuka ajali zisizo za lazima.
POLISI DSM YAWAKAMATA WATUHUMIWA SUGU 103
Jeshi
la Polisi Kanda Maalum Dar Es salaam limefanya msako mkali kuanzia tarehe
02.12.2016 hadi 08.12.2016 na kufanikiwa
kuwakamata jumla ya watuhumiwa sugu 103 wa makosa mbalimbali. Watuhumiwa hao
wamekamatwa maeneo mbalimbali kwa nyakati tofauti tofauti. Wamekamatwa kwa
makosa ya unyang’anyi wa kutumia nguvu, kuvunja nyumba usiku na kuiba, wizi
kutoka maungoni, kucheza kamari, kubughudhi abiria, wizi wa magari, wizi kutoka
maungoni, kutengeneza, kuuza na kunywa pombe haramu ya Gongo, uvutaji bhangi nk
Oparesheni
hii ni endelevu tunawaoba raia wema waendelee kutoa taarifa za uhakika za
kuhusu uhalifu unaotendeka, uliotendeka na unaotarajiwa kutendeka.
NIWATAKIE SIKUKUU NJEMA YA UHURU NA MAULIDI
S.N.SIRRO - CP
KAMISHNA WA POLISI KANDA
MAALUM
DAR ES SALAAM
No comments:
Post a Comment