TUNDULISU AHOJIWA KUHUSU "MTAKATIFU"...
1. Kwanza amehojiwa kwanini anamwita Mheshimiwa Bwana Mkubwa JPM kuwa ni Mtakatifu. Tundulisu amewashangaa Polisi kuwa kwa nini akiita lile jina linalohusiana na udikteta wanamfungulia kesi, Je na hili la Mtakatifu ni shida? Amehojiwa aeleze maana ya Mtakatifu akaeleza ni "asiye na hatia mbele ya Mungu na wanadamu".
2. Kwanza amehojiwa kuhusu kikosi kazi kinachotesa watuhumiwa wanaokuwa chini ya polisi lakini huchukuliwa na kupelekwa kwenye chumba cha mateso na kurejeshwa alfajiri Central Police. Amewaambia Polisi kuwa yeye ameongea na walioteswa na wapo tayari kutoa ushahidi kuhusu ukatili wa kikosi kazi hicho. RCO wa Ilala amekana tuhuma za watuhumiwa kuteswa.
3. Pili amehojiwa kuhusu sakata la kupotea Ben Saanane na polisi wanavyoweza kumtafuta amewaambia watafute mawasiliano yake ya mwisho waseme Saanane yuko wapi.
#Note: Lissu amehojiwa chini ya usimamizi wa Wakili Fred Kiwhelo tangu saa Nne asubuhi hadi saa kumi na nusu jioni hii. Polisi wamefungua jalada la uchunguzi kuhusu maelezo hayo na Tundulisu ameachiwa.
Hii ni Kauli ya Tundu Lissu Baada ya Kutoka Polisi aliposhikiliwa kwa masaa kadhaa kwa mahojiano
Waheshimiwa nawasalimu kwa heshima zote. Muda mfupi uliopita
nimetoka Kituo Kikùu cha Polisi, Central, Dar, nilikokuwa tangu asubuhi.
Niliitwa kuhojiwa juu ya mambo mawili: kauli nilizotoa wakati wa press
conference ya wiki iliyopita kwamba watu wanaomkosoa Mtakatifu Rais wetu
mitandaoni wamekuwa wakikamatwa, kushikiliwa kwa muda mrefu bila kufikishwa
kortini na kuteswa na kikosi kazi maalum kinacho-operate kutoka kwenye nyumba
moja iliyoko Mikocheni, Dar.
Polisi wanadai kauli hizo
ni za kichochezi. Aidha wanadai kumwita Magufuli Mtakatifu Rais ni uchochezi
mwingine. Sababu ya pili ya kuitwa Central ni kutoa taarifa za kusaidia polisi
katika upelelezi wao kuhusu kupotea kwa Ben Saanane. Kuhusu uchochezi,
nimewaeleza polisi kwamba ni kweli kuna kikundi maalum ambacho kinatesa watu
wanaotuhumiwa kwa tuhuma za makosa ya mtandaoni na makosa ya ugaidi na
ujangili. Ushahidi ni mkubwa sana juu ya suala hili. Walioteswa wapo na ndio
waliotueleza mambo mabaya waliyofanyiwa.
Wengine niliwakuta mimi mwenyewe nilipokamatwa Juni mwaka huu na
kulala Central wakati wa Uchochezi One. Kuhusu Mtakatifu Rais, nimewakumbusha
kwamba nilipomwita Dikteta Uchwara walinikamata. Sasa nimemwita Mtakatifu Rais
nayo shida, inakuwaje??? Na by the way, tangu kesi ya Dikteta Uchwara One
ilipoanza, mashahidi wao wameshindwa hata kuieleza Mahakama maana ya maneno
'Dikteta Uchwara.' In short, hakuna uchochezi wowote ambao nimefanya.
Ni mbinu zao tu za kutaka kutufunga midomo ili tusimseme huyu
Mtakatifu wao anayedhani kinachotokwa kinywani mwake ndio sheria ya nchi.
Kuhusu Ben Saanane, nimewaambia timu ya wapelelezi (hawa wako tofauti na
walionihoji kuhusu uchochezi) kwamba kuna kila sababu ya kuamini kwamba kupotea
kwa Ben Saanane kuna uhusiano na wale waliomtumia message kwamba 'his days are
numbered' kwa kuendelea kwake kuhoji uhalali wa PhD ya Magufuli.
Katika mazingira ya sasa
ya kisiasa ambapo kila anayemsema Magufuli vibaya anakamatwa na kuteswa haiwezi
kuwa ajabu kwamba Ben Saanane amepotea katika mazingira ya utata namna hii.
Kitu muhimu hapa ni 'motive', nani atakuwa na sababu ya kumpoteza Ben Saanane.
Walionihoji walikuwa 'very polite', lakini kilicho muhimu zaidi ni kwamba
tuendelee kupaza sauti zetu serikali hii ituambie Ben yuko wapi. Hadi sasa
hawajasema kama wamemkamata na/au wanamshikilia. Hawajasema kama ametoka nje ya
nchi hii au la, na wao ndio wanaodhibiti exit points zote. Hawajasema
mawasiliano yake ya mwisho yalikuwa lini, na nani, wapi na yalikuwa yanahusu
nini. Wao ndio wana technical capabilities za kutuambia majibu ya maswali haya.
Tuendelee kupiga kelele ili watoe actionable information kwa umma kuhusu Ben
Saanane. Baada ya kuchukua maelezo kwa karibu masaa sita wameniachia kwa
dhamana na wameahidi kuniita watakaponihitaji muda wowote. Niwatakieni Merry
Christmas and Happy New Year 2017. Tundu
No comments:
Post a Comment