Imeelezwa kuwa Rushwa
kwa viongozi wa serikali za vijiji na maeneo mengine ndiyo imekuwa chanzo
kikubwa cha migogoro mingi ya ardhi nchini Tanzania ambayo imekuwa ikiibuka
katika maeneo mengi na kusababisha matatizo makubwa yakiwemo vifo na uharibifu
wa mali.
Hayo yameelezwa leo
jijini Dar es salaam katika warsha maalum iliyoandaliwa na serikali kupitia
wizara ya ardhi ambao wamewapa nafasi Shirika lisilo la kiserikali la
TGNP-MTANDAO kuwakutanisha wanajamii mbalimbali kujadili kwa pamoja sera mpya
ya ardhi ambayo inatengenezwa nchini kwa sasa na pia kupitia kwa pamoja sera zilizopo
ili kuona ni jinsi gani wanaweza kurekebisha maswala mbalimbali kwenye sera mpya
ambayo inatengenezwa kwa sasa.
Mwezeshaji Magdalena Rwebangira akitoa mada katika Warsha Hiyo iliyofanyika Jijini Dar es salaam |
Akizungumza katika
warsha hiyo Mwezeshaji wa leo ambaye ni Magdalena Rwebangira amesema kuwa
baadhi ya viongozi wa serikali za mitaa na vijiji wamekuwa wakitumia nafasi zao
kuuza mashamba mara mbili mbili kwa watu tofauti tofauti jambo ambalo limekuwa
likianzisha migogoro mingi kutokana na shamba moja kukutwa na wamiliki Zaidi ya
mmoja.
Amesema kuwa moja ya
maswala ambayo wanayajadili katika semina hiyo ni pamoja na kuona ni jinsi gani
wanaweza kuishauri serikali kutengeneza sera ambayo itakuwa na uwezo wa kuondoa
migogoro mingi ya ardhi nchini ambayo imekuwa ikisababisha matatizo makubwa.
Aidha katika mjadala
huo pia wamejadili kwa kina swala la umiliki wa ardhi nchini Tanzania ambapo
imeonekana kuwa bado watanzania walio wengi hususani wanawake na wajane wa
vijijini wamekuwa wakikosa Fursa ya kumiki ardhi kutokana na Imani walizowekewa
kuwa ardhi itamikiwa na wanaume tu jambo ambalo mwezeshaji huyo amelikataa na
kusema kuwa hata katika Rasimu mpya ya katiba swala la umiliki wa ardhi nchini
limeonyeshwa kuwa ni la kila mtanzania na sio kundi moja la watu.
Nyangi Marwa mwanamama kutoka mkoani Mara Akizungumza na wanahabari |
Katika mkutano huo
ambao ulihudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo wanawake kutoka mikoani mmoja
wapo akiwa ni Nyangi Marwa mwanamama kutoka mkoani Mara ambapo akizungumza na
mtandao huu amekiri kuwa wanawake wengi wa Tanzania wamekuwa hawana uelewa wa
kutosha kuhusu maswala ya umiliki wa ardhi na sera zinazotuongoza jambo ambalo
limezidi kuwafanya kuwa chini ya wanaume katika umiliki wa ardhi nchini
Grace Kisetu kutoka mtandao wa TGNP |
Naye Grace Kisetu
kutoka mtandao wa TGNP nchini Tanzania ambao ndio walikuwa wenyeji wa mkutano
huo amesema kuwa mkutano huo umeandaliwa na Serikali kwa lengo la kuwapa nafasi
wananchi kupitia Mtandao wao kutoa maoni juu ya Rasimu ya sera ya ardhi ambayo
inatangenezwa kwa sasa nchini Tanzania pamoja na kupitia Sera nyingine ikiwepo
ile inayotumika ya mwaka 1995 ili kuona kama kuna mambo ambayo yanafaa kuwepo
katika sera mpya nchini.
Mkutano huo pia
umehudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo wanasheria kutoka wizara ya ardhi
pamoja na maafisa mbalimbali wa ardhi na wadau kutoka mashirika mbalimbali ya
kiraia nchini
No comments:
Post a Comment