Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt Harrison Mwakyembe akizungumza wakati alipokutana na ujumbe wa Msajili wa Mahakama ya Masalia ya Kesi za Mauaji ya Kimbari yaliyotokea nchini Rwanda Dkt. Olufemi Elias aliekaa kulia kwa Mhe. Waziri Mwakyembe |
Waziri wa Mambo ya Katiba na
Sheria Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe amekutana na kufanya mazungumzo na Msajili
mpya wa iliyokuwa Mahakama ya Umoja wa Mataifa ya Masalia ya kesi za mauaji ya
Kimbari yaliyotokea nchini RWANDA (UNITED
NATIONS RESIDUAL MECHANISM FOR INTERNATIONAL CRIMINAL TRIBUNAL- UNMICT) Dkt. Olufemi Elias.
Ugeni huo wa Msajili Dkt.
Olufemi Elias kumtembelea Mhe Waziri Mwakyembe ofisini kwake jijini Dar es
salaam ulikuwa kwa ajili ya kumsalimia na kujitambulisha rasmi kwake kwamba
yupo nchini na ameshaanza kazi yake kama msajili wa mahakama hiyo.
Ugeni huo wa msajili ulimtaarifu
Mhe Waziri kuwa maktaba ya mahakama hiyo iliyoko mjini Arusha inaweza kutumiwa
na wasomi wa sheria nchini hasa wale wanaotaka kufanya utafiti katika masuala
ya mauaji ya kimbari ya Rwanda .
Akizungumza katika kikao
hicho, Mhe Waziri amepongeza ujio wa msajili huyo na timu yake na kumuahidi
ushirikiano zaidi katika kuhakikisha anatekeleza vizuri kazi zake akiwa hapa
nchini.
Kuhusu uwezekano wa kutumia
maktaba ya mahakama hiyo Mhe. Wazri alielezea kuvutiwa kwake na mpango huo na
kuahidi kuwa atakuwa balozi mzuri ambaye atafikisha ujumbe huo kwa shule na
vitivyo vya sheria nchini ili viweze kutumia rasilimali hiyo kwa ajili ya
kuboresha sekta ya sheria nchini.
No comments:
Post a Comment