Nadhra Mresa akikabidhiwa zawadi yake kutoka kwa Yusuph Karimjee wakati wa Hafla Fupi ya kukabidhi zawadi kwa washindi hao. |
Taasisi ya Karimjee
Jivanjee Foundation imewapatia zawadi Diana sosoka na Nadhra Mresa ambao ni
wanafunzi wa shule ya secondary ya wasichana Mtwara kwa kuibuka washindi wa
kwanza kwenye mashindano ya wanasayansi chipukizi Young Scientist Tanzania
(YST) kwa mwaka 2016.
Akizungumza na wahabari
wakati wa Hafla ya kuwaaga washindi hao wanaoelekea katika Jiji la Dublin
nchini Ireland kwa niaba ya mwenyekiti wa KJF Yusuph Karimjee amesema kuwa
wawili hao watapata ufadhili wa masomo wa elimu ya juu pindi watakapohitimu
masomo yao ya kidato cha sita.
Diana sosoka Mshindi wa shindano la wanasayansi chipukizi akikabishiwa zawadi yake kutoka kwa Yusuph Karimjee leo Jijini Dar es salaam. |
Wanafunzi hao
watasafiri kwenda Dublim nchini Ireland leo kwa ajili ya kushughudia mashindano
ya Tafiti mbalimbali ya kisayansi zilizofanywa na wanafunzi wa nchi hiyo,hatua
ambayo itawaongeza ujuzi wanafunzi hao wa mtwara wa namna ya kuboresha mradi
wao.
Mwenyekiti wa taasisi
hiyo ya KJF amesema kuwa wao wanafuraha kubwa kuwa moja kati ya wafanikishaji
wa wanafunzi hao kutimiza ndoto zao za kimasomo hasa kiwango chao cha masomo ya
sayansi jambo ambalo linapiganiwa na dunia nzima kuwa na wanasayansi wengi.
Wasichana hao
walishiriki mashindano ya wanafunzi mbalimbali wanasayansi yaliyoandaliwa na
Taasisi ya young scientist Tanzania TYS Ambapo yalishirikisha wanafunzi kutoka
shule mbalimbali nchini Tanzania wakionyesha ubunifu mbalimbali wa kisayansi
ambao wamebuni.
Wanafunzi hao kutoka
Mtwara secondary waliibuka kidedea baada ya kueleza wazo lao la kutaka
kuwasaidia kina mama wa mkoa wa mtwara kuondokana na umasikini waliokuwa nao
kwa kuwafundisha ufugaji wa kisasa wa kutotolesha kuku ambao wanaweza kuutumia
katika kujikwamua na umaskini ulio mkubwa.
Wakizungumza na
wanahabari wasichana hao wamesema kuwa masomo ya sayansi yamekuwa yakionekana
kama ni magumu sana hasa kwa watoto wa kike jambo ambalo wamesema sio kweli
bali kinachihitajika ni juhudi za kweli na nia ndiyo itakayomsaidia msichana
mwanafunzi kufikia malengo yake.
No comments:
Post a Comment