Ikiwa Tanzania
inatimiza miaka 50 tangu kutolewa kwa azimio la arusha ambalo lilijadiliwa na
kupitishwa na halmashauri kuu ya chama cha TANU iliyoketi Mkoani arusha
hatimaye chama cha Uopiunzani nchini Tanzania ACT WAZALENDO kimetangaza kufanya
mjadala mkubwa wa kitaifa ambao utafanyika Mkoani arusha tarehe 25 March 2017
ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho hayo
ya azimio la arusha.
Akizungumza na
wanahabari mapema leo Jijini Dar es salaam Katibu wa itikadi na uenezi na
mawasiliano ya umma kutoka chama hicho Bwana Ado Shaibu amesema kuwa Mjadala
huo utafanyika kupitia mkutano mkuu wa Kidemocrasia ambapo kwa mujibu wa Ibara
ya 29 ya katiba ya chama hicho cha ACT WAZALENDO ya mwaka 2015 kila mwananchi
anaruhusiwa Kuhudhuria.
Amesema kuwa Mjadala
Huo utakuwa ni Jukwaa la kitaifa kutafakari Mafanikio na mapungufu ya azimio la
arusha na nafasi yake katika Tanzania ya leo,huku akisisitiza kuwa mkutano huo
wa kidemocrasia utajadili nafasi ya siasa za kijamaa na mlengo wa kushoto
Barani Africa na duniani katika zama hizi za kukua kwa kasi kwa siasa za mlengo
wa Kulia.
Pamoja na hayo mutano
huo pia chama hicho kitautumia katika kutafakari dhana ya azimio la Tabora
linalohuisha azimio la Arusha katika mazingira ya karne ya 21.
Mbali na viongozi wa
chama cha ACT WAZALENDO chama hicho kimewaalika viongozi mbalimbali wa kisiasa
duniani na vyama mbalimbali,wawakilishi wa asasi za kiraia,wanazuoni,na
wanaharakati kutoka ndani nan je ya nchi,ambapo chama hicho kimeshatoa mwaliko
na kufanya mazungumzo na vyama vya Labour (Uingereza),Economic Fredom
Fighter-EFF(Africa ya kusini)Die Linke(Ujerumani),na Syriza(Ugiriki)ili
viongozi wao washiriki na kutoa mada kwenye mkutano huo.
Shaibu amesema kuwa
chama hicho pia kimewaalika waliokuwa wanachama wa wa Taasisi ya Ruvuma Development
Asociation (RDA) na wanachi wengine wa kawaida walioishi wakati wa azimio la
arusha ili watoe uzoefu wao.
No comments:
Post a Comment