Maandalizi ya mchezo wa kesho wa kimataifa kati ya Young
Africans ya Tanzania na Ng’aya ya Comoro, yamekamilika kwa asilimia 100.
Timu zote zipo Dar es Salaam, ambako Young Africans wao wameweka
kambi kwenye Hoteli ya Zimbo iliyoko Kariakoo kwenye makutano ya mitaa ya Ndovu
na Nyamwezi, Dar es Salaam.
Kwa upande wa timu ya N’gaya, yenyewe imefikia Hoteli ya
Kaluganje iliyoko Mtaa wa Gerezani, Kariakoo wakati waamuzi kutoka Uganda,
pamoja na Kamishna wa mchezo wanatarajiwa kutua leo.
Mchezo wa marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Young
Africans ya Tanzania na Ngaya ya Comoro hatua ya awali utachezeshwa na Waamuzi
kutoka Uganda ambano ni Alex Muhabi Nsulumbi atayekapuliza filimbi uwanjani,
akisaidiwa na Ronald Kakenya na Lee Okello wakati Mwamuzi wa Akiba atakuwa
Brian Nsubuga Miro huku Kamishna akitokea Afrika Kusini ambaye ni Monnyenyone
Lucas Nhlapo.
Mchezo huo utafanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kama
ambavyo Young Africans walithibitisha CAF majuma mawili yaliyopita kabla ya terehe
ya mchezo huo ambayo ni Februari 18, mwaka huu.
Tumepata taarifa kuwa kuna baadhi ya watu wana mpango wa
kuonyesha mabango yenye ujumbe wa kukashifu Serikali na Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) na wadau wengine.
Tunachukua fursa hii kuonya wanafamilia ya mpira wa miguu
wanaotaka kujihusisha na mipango hiyo, kuacha mara moja kwani vyombo vya dola
vitakuwa makini kuangalia aina yoyote ya utovu wa nidhamu uwanjani.
..…………………………………………………………………………........................
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment