Tarehe
2 ya mwezi wa 4 dunia nzima inaadhimisha siku ya usonji Duniani na kwa hapa nchini
kwetu maadhimisho hayo yamefanyika katika shule ya al muntazir. Yakitanguliwa
na matembezi yaliyoanzia shule ya Al Muntazir ya wavulana iliyopo karibuni na hospital
ya aghakani mpaka shule ya al muntazir
ya wasichana kupitia barabara ya barack obama na kutokea barabara ya umoja wa
mataifa.
Matembezi
hayo yalikuwa na kauli mbiu inayosema kuwa “TUWAPENDE NA TUWALINDE” ikiwa na
maana ya kuwapenda na kuwapatia ulinzi watoto wenye mahitaji maalumu.
Pia
maandamano hayo yaliudhuriwa na Makamu wa Rais mstaafu Dr Mohamed Garib Bilal ambae
pia alikuwa mgeni rasmi wa shughuli hiyo. DR Bilal alipongeza jitihada hizo
zilizofanywa na uongozi wa shule hiyo kwani ni mfano wa kuigwa kwa jamii kwa
kuwa leo hii imeweza kuwakutanisha watoto na wazazi toka sehemu mbalimbali
lengo ni kuwapa elimu jinsi ya kuwalea watoto hawa.
Kuwa
inafahamika kuwalea watoto hawa kunachangamoto nyingi lakini inabidi kuweza
kizikabili kwa kuwa watoto hawa ni zawadi toka kwa mungu na mungu anapima utu
wetu kupitia watoto hawa. Lakini pia sio kuwapenda na kuwatunza tu bali
kuwaweka pamoja na jamii ili wao kuweza kujiona ni sehemu ya jamii na sio
kutengwa kwani wanajiona wapweke.
Na
hii ndio sababu iliyopelekea Khoja Shia Ithal Ashel Mamaat kupitia Centre Board
of Education kuweza kuanzisha shule hizi kwa kuwa waliweza kuona changamoto
hizi. Na kuamua kuanzisha shule hizi lengo ni kuwasaidia vijana hawa wenye
mahitaji maalum mnamo mwaka 2013 na shule ikiwa inapokea watoto kuanzia miaka 3
mpaka miaka 22.
Lakini
pia mgeni Rasmi DR. Bilal aliweza kuchangia kiasi cha shilingi milioni moja
taslimu alizo zitoa hapo akimkabidhi Mwenyekiti wa Khoja Shia Itha ashel Jamaat
central board of education Mr Intiaz Lalji kwa kuweza kuongeza nguvu katika
zoezi la kuwasaidia vijana hao. Huku akiwasilisha mchango Makamu wa Raisi wa
sasa Mama Samia suluhu aliyeweza kutoa mchango wa million 5.
No comments:
Post a Comment