Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya KCB wakishiriki
zoezi la uchangiaji damu.
|
Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Mh. Ummy
Mwalimu (kushoto) akimpongeza mmoja wa wafanyakazi wa Benki ya KCB Bi. Francisca
Alphonce kwa kuwa mmoja wa watanzania waliojitokeza kuchangia damu salama.
|
Wafanyakazi wa Benki ya KCB Bank Tanzania leo wamechangia damu. Hii ni
katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya uchangiaji damu (world blood donor day)
ambayo itaadhimishwa dunia nzima jumatano wiki hii, tarehe 14 Juni.
Akizungumza
wakati wa zoezi hilo ambalo lilihudhuriwa na Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Ummy Mwalimu, Mkurugenzi Mtendaji
wa benki hiyo, Cosmas Kimario alisema kuwa mchango huo upo ndani ya
vipaumbele vya benki katika uwekezaji jamii kwa ajili ya kusaidia
jamii zilizo na uhitaji.
“Benki ya
KCB Tanzania inadhamini uwajibikaji kwa jamii ambayo kwa kiwango kikubwa
inalenga maeneo ya vipaumbele vya Afya, Elimu Mazingira, Ujasiriamali na
malengo yake hasa ni kujikita katika masuala ya ubinadamu” alisema Kimario.
Mkurugenzi
huyo alisema kuwa swala la kuchangia damu ni la muhimu sana kwani kuna
wagonjywa wengi wenye hitaji la damu hivyo elimu juu ya uchangiaji damu salama
ni muhimu kutolewa kwa jamii ili kuifanya jamii kuwa na uelewa mpana juu ya
zoezi hilo.
“Tumeamua
kuandaa uchangiaji wa damu ili kuisaidia serikali katika sekta ya Afya hususani
katika kupunguza vifo vinavyotokana na upungufu wa damu” aliongeza Kimario.
Akizungumza katika zoezi hilo Waziri Ummy Mwalimu aliipongeza Benki
ya KCB Tanzania kwa mchango wake huo na kutoa wito kwa wadau wengine kuiga
mfano wa ukarimu wa Benki hiyo, akibainisha kwamba serikali inahitaji kubwa la
damu hivyo inawahamasisha na kuwakaribisha watanzania wengi zaidi kujitokeza
kuchangia damu na kuokoa maisha kwa kuwa serikali haiwezi kufanikisha malengo
peke yake.
“Nawapongeza sana Benki ya KCB kuwa wakwanza kuanzisha zoezi hili
mwaka huu. Nawahimiza na wengine wajitokeze na waige mfano huu” alisema Waziri.
Zoezi
hilo lilifanyika makao makuu ya ya Benki ya KCB, Oysterbay jijini Dar es
Salaam. Wakizungumza mara baada ya kuchangia damu kwa
hiari baadhi ya wafanyakazi wa benki ya KCB wamesema kuwa zoezi hilo limeenda
vizuri na kuwa suala la kuchangia damu ni lamsingi sana kwani wapo watu
waliopungukiwa damu, wagonjwa na wanaopata ajali na kuhitaji damu.
Kwako wewe mtanzania jiulize kwanini usichangie damu kuokoa maisha
ya watanzania wengine.
|
No comments:
Post a Comment