Kampuni ya vifaa vya teknolojia ya Samsung Tanzania
imeanzisha mfumo mpya wa uwekaji stika mbili katika bidhaa zao kwajili ya utambuzi
wa bidhaa halisi ikiwa ni njia ya kupambana na bidhaa feki hapa nchini.
Meneja bidhaa wa kampuni ya Samsung Tanznia bw. Elias Mushi akiongea na waandishi wa habari ambao hawapo pichani mapema leo makao makuu ya kampuni hiyo. |
Akitoa ufafanuzi mbele ya waandishi wa habari katika makao makuu ya kampuni hiyo Jijini Dar es
salaam,Meneja bidhaa Bw.Elias Mushi amesema stika hizo zitasaidia kutambulisha
bidhaa halisi ya kampuni hiyo lakini sambamba na njia mojawapo ya kupambana na
bidhaa feki kwani bidhaa hizo
zinahatarisha afya za watumiaji na mahitaji ya bidhaa bora na halisi
zinaongezeka hivyo wanaendelea kufanya jitihada zaidi katika kukidhi matakwa ya
wateja ulimwenguni na Tanzania kwa ujumla.
“Ukizingatia bidhaa feki zina hatarisha afya ya
watumiaji,mahitaji ya bidhaa bora na halisi yanaongezeka kwa kasi kila
kukicha,Samsung tumeendelea kufanya jitihada
zaidi katika kukidhi matakwa ya wateja wetu ulimwenguni na Tanzania kwa
ujumla”alisema
Aidha,Meneja amesema wameongeza alama mpya katika bidhaa zao
ambapo stika hizo mbili zitawasaidia wateja kutambua bidhaa feki sokoni,kwani
stika moja itakua ni stika msambazaji na ya pili itakua stika inayotambulisha
bidhaa halisi ya Samsung.
Meneja wa Pyramid Consumers LTD Kareen Babu akiongea na wanahabari (hawapo pichani) mapema leo jijini Dar es salaam. |
Pia, Bw.Mushi aliwatambulisha Tanzania Pyramid Consumers
ltd,kuwa ndio wasambazaji wao ambao wameingia nao ubia kwa lengo la kurahisisha
upatikanaji wa bidhaa za kisasa za kieletroniki za Samsung ndani ya Tanzania
zikiwemo Tv,Friji,viyoyozi,mashine za kufulia na macrowave huku akiahidi kuwa
wapo mbioni kutambulisha bidhaa mpya toka kampuni hiyo.
Sambamba na hilo,kampuni ya Samsung Tanzania wamezindua
kampeni ya “Nunua ,sajili, Na
Ushinde “ itayoendeshwa kwa mwezi mmoja nchi
nzima ikiwa ni kiunganishi cha kupeleka elimu kwa wateja wao na kupata uzoefu
wa kuitambua bidhaa halisi ya kampuni hiyo, kabla ya kuendesha bahati nasibu
ambayo washindi watapata bidhaa bora zenye waranti ya miezi 12 kila siku toka
samsung kwa muda Wa mwezi mmoja ikiwa watajisajili kupitia namba za bidhaa(serial
number) walizonunua kwenda 0798 222333.
No comments:
Post a Comment