Diwani wa kata ya Vingunguti ambae pia ni Naibu Mstahiki
Meya Manispaa ya Ilala Bw. Omary Kumbilamoto alifanya mkutano wa adhara na
wananchi wake lengo likiwa ni kukamilisha ahadi zake zote alizoziahidi kipindi
anaomba kura.
Diwani wa kata ya Vingunguti ambae pia ni Naibu Mstahiki Meya wa Ilala Mh. Omary Kumbilamoto akiongea na wananchi wa kata hiyo mapema jana jijini Dar es salaam. |
Kwenye mkutano huo uliokutanisha viongozi mbalimbali wa kiserikali, wamichezo na wavyama tofauti tofauti vya siasa kwa kuweza kumtia moyo kiongozi huyo ili azidi kufanya kazi nzuri kwenye kata yake na taifa kwa ujumla.
Naibu mstahiki Meya wa jiji la Dar es salaam Mh. Mussa Kafana akikabidhi zawadi ya jezi kwa moja ya makocha wa timu za vingunguti. |
Diwani wa viti maalum kata Upanga Mh. Rukia Mohamed akikabidhi zawadi ya jezi kwa mmoja wa viongozi wa timu zinazopatikana kata ya Vingunguti |
Diwani Kumbilamoto alipongeza jitihada za serikali za
kutunza mazingira na kwa hili aliweza kuvirejesha upya Vyoo vilivyojengwa kwa
msaada wa Benki ya dunia na kushindwa kutumika kwa kukosa maji, ambacho choo cha
kwanza kipo eneo la Machinjioni na cha pili kipo eneo la Relini hivyo
akishirikiana na wadau mbalimbali wameweza kuviwekea maji na kwa sasa
vinatumika.
Baadhi ya wakazi wa kata ya Vingunguti wakifurahia baada ya kukabidhiwa kadi za chama cha CUF |
Na kufikia leo diwani ndipo anakuja kumalizia ahadi yake ya mwisho kwa kuwa aliahidi vitende kazi wa wanamichezo ikiwemo jezi na mipira kwa wachezaji wa timu za vingunguti.
No comments:
Post a Comment