Emirates imewapa baadhi
ya familia za kitanzania ladha ya ushindi wa usafiri wa anga wakati walipohudumia
kundi la wazazi na watoto wao katika moja ya sinema kali ya Despicable Me 3.
Sinema mpya iliyotoka katika anga ya dunia- karibia watoto 30 na wazazi wao na
walezi walihudhuria uzinduzi huo uliofanyika Mlimani City Mall IMAX tarehe 8
Julai 2017 kuangalia sinema bora uliyovuta hisia za wengi ikifatiwa na chakula
cha mchana sehemu hiyo hiyo iliyoandaliwa na mwenyeji mkurugenzi wa Emirates
Tanzania, Rashed Alfajeer.
Emirates pia ilipata uzoefu wa familia katika
kutangaza ofa ya 50% katika daraja la uchumi kati ya abiria 2 - 8 kusafiri wote
katika sehemu 21 zilizopendekezwa kama Uarabuni, Ulaya vile vile Marekani
kusini na kaskazini. Hiyo ofa ni kati ya tarehe 6 na 14 julai 2017 na za nje
kati ya tarehe 6 julai na 10 Disemba 2017.
Rashed Alfajeer,
Mkurugenzi Mkuu wa Emirates Tanzania alisema: " Emirates ipo kwa ajili ya
kutoa thamani kwa pesa na wamejihakikisha kutoa huduma iliyo bora angani mpaka
ardhini na hakuna tofauti linapokuja swala la familia katika kusafiri. Kwa
watoto, lazima wawekwe huru na waburudike na kuwajali kwa kuwapa wigo mpana
katika kuchagua sinema na programu ili kukithi mahitaji yao".
Ofa hii maalum inatoa
nafasi kubwa kwa familia kuwa na likizo ya pamoja sehemu mbali mbali kwa
gharama nafuu kwa muda uliowekwa tu na kuongeza wakati wakisafiria na Emirates,
familia itarajie kupata wigo mpana wa program za watoto ikiwa na channeli 90
mahususi kwa ajili ya kuwaburudisha watoto ikiwamo pamoja na sinema bora na
programu za TV kutoka Disney, Cartoon Network, Cbeebies Na Nickelodon na
nyingine nyingi. Chakula pia upewa kipaumbele sana pindi abiria wawapo angani
kwenye Emirates. Watoto wenye umri kati ya miaka 2 na 12 hupewa chakula maalum
wakihudumiwa katika vyombo vya kisasa wakiwa na staff pamoja na marubani. Wasafiri
wenye ugunduzi wachache wanaweza kupata marafiki wapya pindi wawapo safarini,
kuna blanketi kwa ajili ya kujifunika na kuweza kujiburudisha na majarida yanayokuja
Dar Es Salaam kila siku. Ndege ya EK 0725 inatoka Dubai saa 10:25 na kufika Dar
Es Salaam saa 14:50. Ndege inayorudi EK 0726 inatoka Dar Es Salaam saa 16:45 na
kufika Dubai saa 23:20.
No comments:
Post a Comment