Leo ikiwa ni tarehe 27 mwezi wa 7 ni mwanzo wa ziara ya Katibu Mkuu wa wizara ya Habari Sanaa Utamaduni na michezo Mh. Elisante Ole Gabriel
akitembelea vyombo mbalimbali vya habari vya hapa jijini Dar es salaam.
Ziara hiyo iliyoanza kwenye kituo cha Efm radio pamoja na
TVE vilivyopo Kawe jijini Dar es salaam lengo la ziara hiyo ni kuangalia ufanisi
pamoja na kubadilishana mawazo na wafanyakazi wa vyombo hivyo.
Akiongea kwenye mkutano mdogo uliofanyika kwenye makao makuu
ya Efm Mkurugenzi Mtendaji wa Efm Bw. Denis Busurwa alisema kuwa kwa sasa Efm
inasikika kwenye mikoa sita ikiwa Dar es salaam, Mwanza, Mbeya, Mtwara, Pwani
na Tanga.
Na lengo likiwa ni kufika mbali zaidi ya hiyo mikoa waliyopo na
kwa sasa wamefanikiwa kuajiri vijana 110 na kati ya hao asilimia zaidi ya 99 ni
Watanzania na kwa upande wa TVE kutokana imeanza hivi karibuni inaajumla ya
wafanyakazi 20 lakini lengo ni kuajiri
wengi zaidi ili kusaidia kutoa ajira kwa vijana Wakitanzania.
Lakini pia mkurugenzi mtendaji wa Efm alimuomba Mh. Elisante mambo kadhaa ikiwa zinapotokea nafasi za vijana kwenda kujiendeleza nje ya nchi(scholarship) zinapotokea waweze kupatiwa na wao au kwa kuweza kupewa kipaumbele ili vijana wao wakajifunze vitu vingi zaidi kuhusu taaluma yao.
Na pia katika kuunga mkono serikali ya awamu ya tano na
kauli mbiu yake ya serikali ya viwanda wao kama Efm na TvE kwa pamoja wanaomba
kushirikiana serikali ili kuangalia wafanye nini ili Agenda hii iweze kuwa kubwa
zaidi na isimamiwe kikamilifu.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Habari Sanaa Utamaduni na Michezo Mh. Elisante ole Gabriel alisema
mambo mbalimbali waliyoyaomba atayachukua na ataenda kuyafanyia kazi na alipenda
kuwaomba uongozi wa TvE na Efm kujitahidi kufika na mkoa wa Dodoma kwa kuwa kwa
sasa fursa nyingi zimehamia Dodoma ikiwemo serikali yenyewe.
Na alipongeza jitihada za uwekezaji mkubwa uliofanywa na Efm kwani kwa watu
wengi udhania kwamba Efm ni kitu kidogo lakini kwa yeye amegundua kuwa ni
taasisi kubwa iliyowapa ajira vijana wengi wa kitanzania kupitia vituo vyake vya Efm na TvE.
Lakini pia bw. Elisante Ole Gabliel aliuomba uongozi wa Efm kuwajali
wafanya kazi wake ili waweze kupata matunda mazuri zaidi na kwa kuwa wao
wanategemeana kwani bila wafanyakazi hakuna radio na bila radio hakutakuwa na
haja ya wafanyakazi.
Na kitu kingine alikipenda kwa media hiyo ni kuwa na maadili
mazuri na miiko ya kazi hali inayofanya ufanisi kuwa mkubwa mahali hapo na kuwa
wanakubali kurekebishwa pale wanapokosea.
Na Mh. Elisante alipenda kutoa rai kwa wafanyakazi kufanya
kazi kwa bidii kwani ndio msingi wa maisha yao na pia inasababisha Efm na TvE wigo wake kuongezeka na wao kupata sifa na maslahi mazuri kwani uzalishaji ukiwa mkubwa hata
maslihi yao yatakuwa makubwa.
Katibu mkuu wa wizara ya Sanaa Utamaduni na Michezo Mh. Elisante ole Gabriel akkiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Efm pamoja na TvE |
Pia kiongozi huyo alipenda kuwasihi kuwa ni watu wa kujari
muda kwani muda ndio kila kitu na wakiweza kulikabili swala hilo itapunguza majukumu yasiyo ya lazima ya kiongozi kuangali muda ambao wafanyakazi wanafika.
Na jambo la mwisho aliwasihi kuweka Uzarendo mbele kwani wao
ni tegemeo kwa Taifa hivyo wao wakitetelesha Amani iliyopo nchini wataleta madhara makubwa kwa
taifa na pia hata maafa yakitokea hata na wao hawata nusurika kwani na wao ni
sehemu ya Tanzania.
Katibu mkuu wa Wizara ya Habari Sanaa Utamaduni na Michezo akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Efm Radio mapema leo jijini Dar es salaam |
Mkurugenzi Mkuu wa Efm Radio Francis Ciza akipeana mkono na katibu mkuu wa Wizara ya Habari Sanaa Utamaduni na Michezo Mh. Elisante ole Gabliel ikiwa ni baada ya ziara yake aliyoifanya Efm na TvE mapema leo jijini Dar es slaam |
No comments:
Post a Comment