Leo ikiwa ni
tarehe 5 ya mwezi julai taasisi inayotoa kozi za kiingereza na kuunganisha watu
kupitia ubunifu pamoja na utamaduni toka nchini uingereza ya British Council. Leo
imefanya mkutano na waandishi wa habari lengo likiwa ni kuwafahamisha nini
wamekuja nacho kwa msimu huu wa saba saba.
Akiongea na waandishi wa habari mapema leo Mkurugenzi mkazi wa British Council nchini Tanzania Bi. Angela Hennelly alisema kuwa wataendelea kushirikiana na taifa la Tanzania kwa wananchi wake kuhakikisha wanafahamu lugha hiyo ambayo imekuwa ni lugha ya kibiashara na kutumika maeneo mengi zaidi duniani.
Na kuendelea
kusema kuwa “Tunaipenda serikali ya Tanzania, kwa kuwa britishi council ipo
hapa kwa sasa ni takribani miaka 47 tunasaidiana katika kusimamia mitihani
mbalimbali pamoja na kutoa kozi za kiingereza” alisema Angela Hennelly
Baadhi ya vijana walioudhuria zoezi hilo la kufanya mtihani bure kupitia banda la British Council lililopo kwenye hema la Jakaya Kikwete mapema leo Saba Saba jijini Dar es salaam |
Akiongezea mkurugenzi
wa biashara na maendeleo Bi. Amata Bosco alisema kwa sasa British Council
inatoa ofa kabambe kwa wateja wake ya kufanya mtihani bure kabisa kwa msimu huu
wa Saba Saba ambao mtihani huo kwa kawaida unalipiwa shilingi elfu 48 hivyo
ukiwahi ndani ya Saba Saba utafanya bure kabisa bila malipo yoyote.
“Mtihani huo
unakuwa ni kipimo cha kufahamu mwanafunzi anauwezo gani wa kufahamu lugha hiyo kabla
ya kujiunga na kozi ya kiingereza na baada ya hapo mwanafunzi anatakiwa kwenda
makao makuu ya British Council yaliyopo mtaa wa Ohio/Samora evenue kwa ajili ya
kuanza kozi itakayoanza tarehe 24 mwezi huu wa 7”. alisema Amata
Lakini pia jambo lingine zuri ni wanamshukuru Rais
wa Jamuuri ya Muungano wa Tanzania Mh. John Pombe Magufuri kwa kuongeza muda wa
kuwepo mahali hapo mpaka july 13 hivyo wananyongeza ya siku 5 za kuwepo Saba Saba.
Na kwa hiyo wanawaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi kwani hawajachelewa
kuwahi ofa hiyo ambayo ni maalum kwa ajili yao.
Wananchi mbalimbali waliotembelea banda la British Council kujipatia huduma mbalimbali zinazopatikana kwenye banda hilo mapema leo jijini dar es salaam |
No comments:
Post a Comment