TGNP mtandao ipo kwenye maandalizi ya Tamasha la 14 la Jinsia
litakalo fanyika tarehe 5 mwezi 8, 2017. Tamasha hilo linalofanyika kila baada
ya mwaka mmoja na linawakutanisha wadau mbalimbali toka toka Serikalini, vituo
vya taarifa na maarifa, Club za shule tofautitofauti na wanaharakati mbalimbali
ngazi ya kata mpaka taifa na wenyeji washiriki wa semina za jinsia(GDSS).
Akiongea kwenye semina jana jumaa tano Bi. Anna Sangai
alisema kuwa Tamasha hilo ni la wazi na linawakaribisha watu wa aina zote kwani
hakutakuwa na kiingilio hivyo watu wajae kwa wingi kuja kujionea bidhaa
mbalimbali za Tanzania na kupata elimu juu ya ukatili wa kijinsia.
Na kauli mbiu ya mwaka huu ya Tamasha hilo inasema “Mageuzi
ya mfumo kandamizi kwa usawa wa jinsia na maendeleo endelevu”
Bi. Anna Sangai akitoa maelekezo kwenye semina ya wanaharakati wa maendeleo jana kwenye Ofisi za TGNP Mtandao jijini Dar es salaam |
Lengo kuu la tamasha hilo ni kusherehekea mafanikio,
kujadili changamoto na kubadilishana uzoefu kutokana na harakati wanazozifanya
ndani ya muda husika, hivyo wanapokutana inakuwa wakati muafaka wa kupata
mrejesho wa kile walichokivuna au wapi wamekwama ndani ya mwaka uliopita.
Miongoni mwa malengo mengine ni kujadili Mikataba ya kimataifa
amabyo serikali imeingia na kuangalia kama
utekelezaji wake unafanyika juu ya haki za watoto na wanawake, pamoja na
upatikanaji wa huduma muhimu za jamii kama Maji, Elimu, Afya na mengineyo.
Na kwenye Tamasha wageni watakaohudhuria wataweza kupata Elimu
bure, Burudani ya ngoma, Ngonjera , Mashairi, Maigizo maonesho ya bidhaa
mbalimbali pamoja na makablasha yenye mafunzo mbalimbali ya kupinga ukatili wa
kijinsia na utatuzi wake.
Baadhi ya washiriki wa Semina za maendeleo wakifuatilia kwa umakini semina iliyofanyika mapema jana jijini Dar es salaam |
Lakini pia Bi. Anna Sangai alisisitiza kwa kusema kuwa
safari hii wanahitaji bidhaa zinazotengenezwa kwa kazi ya mikono za Watanzania
na siyo kuleta bidhaa za viwanda vikubwa au za kutoka nje ya nchi, kwani lengo
la tamasha hili ni kutangaza na kukuza soko la bidhaa za ndani kwani watakuwepo
wageni toka mataifa mbalimbali ya jirani.
Na kwa wajasiriamali watakaobahatika kuleta bidhaa zao mwaka
huu watapata bahati ya kutembelewa na SIDDO kwa ajili ya kupewa utaalamu wa
kuboresha bidhaa zao, pamoja na TBS kwa ajili ya kuwapa maelekezo yakufanya
namna ya kufungasha ili waweze kuingia kwenye soko la ushindani la bidhaa za ndani
na nje ya nchi.
Baadhi ya wasiriki wa Semina za maendeleo (GDSS) |
Na kwa watakao hitaji kupeleka bishaa zao kwenye maonesho
hayo ambao ni nje ya wanaharakati wa semina za jinsia(GDSS) wanaombwa
kuwasilisha maombi yao mapema kwa kufika makao makuu ya mtandao wa jinsia TGNP
yaliyopo mabibo karibu na chuo cha NIT jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment