Mtandao wa kijinsia wa TGNP umeendesha semina kwa wanaharakati wake
ambapo wameshauri kutumia vizuri vyombo vya habari ili kupaza sauti juu ya
changamoto zinazoikabili jamii ili hatua stahiki zifuatwe katika kuzitatua
changamoto hizo.
Muhariri wa gazeti la Mwanahalisi Bi. Pendo Omary akitoa elimu kwa wanaharakati jinsi ya kutatua changamoto mbali mbali zinazoikabiri jamii kwa kutumia vyombo vya habari. |
Ushauri huo umetolewa leo na muhariri wa gazeti la mwanahalisi,ambaye
pia ni mwanaharakati wa mtandao huo Bi.Pendo Omary wakati wa semina ya mafunzo iliyoendeshwa na
mtandao huo katika ofisi zake za mabibo Jijini Dar es salaam.
Bi. Pendo amesema kuna fursa nyingi za kutumia kwenye vyombo vya habari
ambazo wanaharakati wanaweza kuzitumia katika kuzungumzia kero ama changamoto
ili taasisi husika au serikali iweze kuzipata na kuzitatua kwa wakati.
Wanaharakti mbalimbali wakifuatilia semina kwa umakini iliyoandaliwa na Mtantao wa jinsia TGNP. iliyofanyika mapema jana jijini Dar es salaam |
''kuna fursa nyingi sana kupitia vyombo vya habari ambazo zitaweza
kusaidia katika kupaza sauti juu ya
mambo mbali mbali ikiwemo unyanyasaji na ukandamizwaji wa wanawake
ambapo ndipo sehemu kubwa inatuhusu kama wanaharakati''alisema.
Akizitaja fursa hizo kuwa ni pamoja na uandishi wa barua kwa wahariri na
maoni uchapishwa katika kurasa za magazeti na kusomwa na watu wengi katika
jamii,Bi. pendo pia alielezea juu ya upigaji simu moja kwa moja wakati wa
vipindi vya redio kuwa ni njia inayosaidia katika kupaza sauti juu ya
changamoto zinazoikabili jamii lakini pia ni
moja ya njia ya kuendeleza mapambano juu ya mambo tofauti ikiwemo unyanyasaji na ukandamizaji
wa wanawake.
Muhariri wa gazeti la Mwanahalisi Bi. Pendo Omary akitoa elimu kwa wanaharakati mbalimbali jana jijini Dar es salaam |
Aidha,aliwaasa wanaharakati kutokua waoga wa kuzungumza ukweli kupitia
vyombo hivi kwani ni jukwaa lao katika kufikisha taarifa zinazolenga kuibua
changamoto katika jamii zao licha ya kuwa na ukandamizwaji wa uhuru wa
kujieleza,rushwa zinazotolewa na baadhi ya viongozi ili kuwaziba midomo
wananchi na hata kuhojiwa na vyombo vya usalama pindi watapofahamu kuwa
zimetolewa taarifa ambazo hazikupaswa zitoke.
Pia,Bi pendo aliwatahadhalisha wanaharakati hao kutotoa taarifa zenye
lengo la kejeli,uchochezi baina ya mtu na mtu au kikundi,kumdhalilisha mtu kwa
lengo la maslahi binafsi au kundi la watu kwani kitendo hiko kitaweza
kuhatarisha usalama wake na lengo la fursa ya matumizi ya vyombo vya habari
itakuwa haijatimizwa.
No comments:
Post a Comment