Katika
kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa na Utambulisho wa Kudumu hasa katika
mitandao,serikali imewataka watanzania kujenga utamaduni wa kutumia Rajisi ya
Tanzania (Domain) ambayo ni .TZ badala ya kuendelea kutumia Domaini za mataifa mengine
bila kunufaika na matumizi hayo.
Akifungua
mkutano wa Jumuiya ya watoa Huduma kwenye mitandao ulioshirikisha wamiliki wa
Rajisi mbalimbali Africa kama .ke, .tz,.uk na nyingine Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin
Ambandusi Ngonyani amesema kuwa Nchini ya Tanzania imekuwa
nyuma sana katika kutumia Rajisi yake ya nyumbani ambayo ni .TZ ukilinganisha
na mataifa yanayotuzunguka kama Kenya na mengine jambo ambalo linatajwa
kuendelea kupoteza utambulisho wa Taifa letu katika mitandao.
Naibu
Waziri huyo amesema kuwa mpaka sasa nchini Tanzania watumiaji wa mtandao ambao
wamejisajili katika matumizi ya Rajisi ya nyumbani yani .TZ wanafikia elfu 14
ukilinganisha na majirani zetu Kenya ambao wanafika elfu 60, ambapo amewaasa
watanzania kijijengea utamaduni wa Kutumia utambulisho wa nyumbani.
Ameeleza
kuwa matumizi ya Rajisi ya Nyumbani yana manufaa makubwa sana kwa watanzania
hasa wafanyabishara ambao wanafanya biashara kimataifa kwani itawajengea
kuaminika na wateja wao kwa kuwa wanatambulika nchi wanayotoka tofauti na
kutumia Rajisi za mataifa mengine ambapo wateja watashindwa kuelewa wewe
unatoka nchi gani kutokana na Rajisi yako.
Mkurugenzi Mtendaji wa TZNIC ambao ndio wanaohodhi Rajisi ya .TZ akizungumza na wanahabari kuhusu mambo mbalimbali yatakayojadiliwa katika mkutano huo |
Akizungumzia
Rajisi ya Tanzania na matumizi yake amesema kuwa kwa sasa Rajisi ya .TZ ambayo
ndiyo Rajisi maalum ya watanzania inatolewa na TZNIC ambao wanatoa kwa gharama
za zisizozidi elfu 25 kwa mwaka ambapo amesema kuwa Gharama hizo ni kwa lengo
la kusaidia kujiendesha wakati wanaanza kwa kuwa bado hawaajaanza kupata
matangazo huku akiweka wazi kuwa kadiri muamko wa watanzania utakavyozidi kuwa
mkubwa gaharama hizo zitapungua kwa kiasi.
Akizungumza
nje ya Mkutano huo Mkurugenzi Mtendaji wa TZNIC ambao ndio wanaohodhi Rajisi ya
.TZ Eng.Abibu Ntahigiwe amesema kuwa Lengo kuu la mkutano huo ni kujenga
ushirikiano wa karibu baina ya wamiliki wa Rajisi afrika pamoja na
kubadilishana uzoefu kuhusu maswala ya mitandao,ambapo mkutano huo unafanyika
Tanzania ukiwa ni mkutano wa Tano
kufanyika Barani Africa.
No comments:
Post a Comment