Kituo chako bora cha matangazo Efm radio kinakuletea tamasha
la kila mwaka lijulikanalo kama Muziki Mnene amabalo litazinduliwa rasmi siki
ya jumamosi ya tarehe 28/o8/2017 katika mkoa wa Tanga 103.3 fm.
Meneja mkuu wa Efm na Tv E Bw. Denis Busulwa akiongea na waandishi wa habari mapema leo makao makuu ya Efm yaliyopo Kawe jijini Dar es salaam |
Akiongea kwenye mkutano na waandishi wa habari Meneja mkuu
wa Efm na Tv E Bw. Denis Busulwa alisema tamasha la Muziki Mnene mwaka huu litafanyika
kwa muda wa wiki 10 amabao ni sawa na miezi 2 na wiki 2 ambapo muziki utapigwa
katika viwanja vya mkoa wa Tanga,Mbeya, Mwanza, Mtwara na katika Bar mkoa wa Dar es salaam na Pwani.
Muziki Mnene mwaka huu itaenda sanjari nan akampeni ya NJE
NDANI ambapo vipindi vinne vitarushwa moja kwa moja katika mtaa husika kwa siku
ya ijumaa, na vipindi hivyo ni Joto la asubuhi, Sports headquarters, Uhondo na
Ladha 360. Kipindi cha Funga mtaa kitarushwa siku ya jumamosi pamoja na
burudani itakayotolewa na RDjs wa Efm na kutakuwa na Jogging asubuhi, Singeli
michano kutafuta wasanii wenye vipaji vya muziki wa singeli, mpira wa miguu kati ya timu ya Efm na
Maveteranis/ timu za mkoa katika maeneo husika.
Msemaji mkuu wa Noah Furnishing Bw. Lumumba Farhani akitoa ufafanuzi wa jambo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika mapema leo makao makuu ya Efm Radio Kawe jijini Dar es salaam |
Tamasha la Muziki Mnene vilevile litaenda sanjari na kampeni
ya ugawaji mafuta katika mikoa ya Tanga, Mtwara, Dar es salaam na Pwani, ambapo
vyombo vyote vya moto vyenye stika ya masafa ya Efm radio vitapata mfuta bure
kama ambavyo zoezi hilo lilivyofanyika katika mikoa ya Mbeya na Mwanza.
Bila kuwasahau wadhamini wa tamasha la Muziki Mnene amabao
ni Noah Furnishing pamoja na kampuni ya Biko Tanzania ambapo biko itakuwa
ikichezesha bahati nasibu kwenye kila sehemu ambapo Muziki Mnene utakuwepo na
mshindi wa kwanza atapata zawadi ya donge nono na wakifuatia na washindi wa
papo kwa hapo hadi shilingi milioni moja.
Mkurugenzi wa Masoko wa Biko Tanzania Bw. Goodhope Heaven akitoa ufafanuzi wa jambo fulani katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika mapema leo jijini Dar es salaam |
“Lengo la tamasha hili ni kukutana na kuwashukuru wasikilizaji wetu kwa kuipokea na kushirikiana nasi hadi sasa katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam, Pwani pamoja na mikoa tajwa hapo juu ambayo Efm inasikika , ikiwemo pia kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili katika maeneo yao” alisema Denis Busulwa.
Balozi mpya wa Noah Furnishing Swebe Santana au Rais wa wanaume akiongea na waandishi wa habari kwenye mkutano uliofanyika mapema leo Kawe jijini Dar es salaam |
No comments:
Post a Comment