TGNP Mtandao katika kutambua nafasi ya wanajamii imetoa
nafasi maalum kwa watu waliofanya mambo
makubwa kwenye jamii yao na mchango wao haukutambulika, hivyo watapewa nafasi
ya kuadithia simulizi zao mpaka kufikia mafanikio aliyoyapata.
Hayo yalizungumzwa jana kwenye semina ya jinsia na maendeleo (GDSS)
ilifanyika mapema kwenye ukumbi wa
mtandao huo Mabibo jijini Dar es salaam.
Akiongoza semina hiyo afisa programu wa TGNP Mtandao Bw. Deogratius
Temba alisema kuwa lengo kuu la tamasha hilo ni kusherekea mafanikio na
kuangalia changamoto mbalimbali zinazowakabili kwenye harakati zao.
Amesema kuwa Wametoa nafasi hiyo kwa wanajamii na washiriki
wa semina za jinsia na maendeleo kuwapa
nafasi ya kusimulia stori za maisha yao kwa wale waliopitia magumu mpaka
kufanikiwa na kutoa zawadi kwa waliofanya vizuri katika harakati za jinsia na
maendeleo.
Kwa washiriki wa semina za jinsia na maendeleo na wanajamii
kwa ujumla watapata nafasi ya kushiriki kwenye mjadala wa wazi na baadae
kushiriki kwenye warsha ndogo ndogo
zitakazofanyika kwenye tamasha hilo.
Aidha ameongeza kuwa kwenye warsha hizo kutakuwa na mada mbalimbali
zinazoongoza kila warsha kama mjadala wa Maji, Elimu, Ardhi, Mazingira Madini,
Mabadiliko ya tabia ya nchi, Afya na mengine mengi.
Amesisitiza kuwa warsha hizo zitaongozwa na idara mbalimbali za serikali pamoja
na mashirika rafiki na Mtandao wa Jinsia(TGNP) kama TAMWA, MEWATA, WLAC, Plan
International, Haki elimu, Mfuko wa wanawake, Haki ardhi, VIWATA na mashirika mengine mengi.
No comments:
Post a Comment