MWANAMITINDO ‘the big name’ Bongo, Jokate Urban Mwegelo ‘Kidoti’, wikiendi iliyopita alinaswa na mapaparazi akiwa amejibebisha (jokate ajibebisha kwa henry) kwa staa wa soka wa mamtoni, Thierry Henry ambae ni mchezaji wa zamani wa Timu ya Arsenal ya England.
Kwa mujibu wa picha hizo zilizosambaa mitandaoni jana, wawili hao walikutana Johannesburg nchini Afrika Kusini katika Ligi ya Mpira wa Kikapu (NBA) ya Afrika kwa mwaka 2017.
Jokate ambaye ni Balozi wa NBA kwa upande wa Afrika alihuduria mashindano hayo yaliyokutanisha timu za NBA kwa wachezaji wenye asili ya Afrika na wale wa mataifa mengine. Katika hali iliyoibua sintofahamu na maswali kibao, katika picha moja alionekana na mavazi tofauti na yale aliyoonekana nayo awali, lakini picha zote akiwa na Henry katika sehemu iliyosadikiwa kuwa ni hotelini huku wakionekana ni wenye furaha.
Picha hizo zilivuja ikiwa ni miezi kadhaa tangu Jokate alipoonekana na mastaa wengine wakubwa wa muziki nchini Marekani, Jay-Z na Beyonce.
Kupitia ukurasa wake jana, Jokate alitundika picha hizo na kuandika: “Nahamia Arsenal rasmi, naomba ushauri, lakini naambiwa Arsenal ni stress tupu.”
VIPI KUHUSU UHUSIANO WAKE NA ALIKIBA?
Kwenye suala la uhusiano wa kimapenzi, bado penzi la Jokate na mwanamuziki Ali Kiba ni kizungumkuti ambapo wamekuwa wakiachana na kurudiana.
No comments:
Post a Comment