Kampuni ya simu za mkononi ya itel kwa kushirikiana na
balozi wake Irene Uwoya, imetoa Msaada wa vifaa vya masomo pamoja na bidhaa za
mahitaji ya msingi kwa wanafunzi 76 wenye mahitaji maalum katika shule ya
msingi Uhuru jijini Arusha.
Afisa hABARI WA itel Fernando Wolle Akizungumza katika hafla hiyo |
Akikabidhi vifaa hivyo mwishoni mwa wiki balozi wa itel
Irene Uwoya alisema jamii inapaswa kufahamu kuwa wapo wahitaji ambao wanataakiw
kukumbukwa na jamii yao iliyowazunguka.
“Napenda kuwaasa Watanzania wenzangu kwamba kuna watu
wanahitaji elimu lakini kuna vitu wanakosa vya kuwasaidia wapate hiyo elimu,
suala la msingi ni kujitahidi mahali sahihi pa kupeleka msaada huo, sisi kama
itel, tumeona ni vyema tuanze kuleta
hapa lshule ya Uhuru lakini tutaendeleza jitihada hizi kwasababu tunaamini
elimu ndio kila kitu” Alisema Uwoya.
Balozi wa Itel Tanzania Msanii Irene Uwoya akimkabishi Mwalimu mkuu shule ya msingi Msingi Uhuru jijini Arusha.Zurina Rajabu msaada wa Vifaa mbalimbali |
Naye Meneja masoko wa
kampuni ya itel kanda ya Kaskazini Bwana
Noel Mgasa alisema wameamua kutoa msaada
huo kutokana na shule hiyo kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi wenye uhitaji.
“Kimsingi tumeamua kutoa msaada huu kwa kuona umuhimu wa jitihada
zinazofanywa na walimu wa shule ya msingi Uhuru na wadau wengine wanaojali
umuhimu wa elimu,na sisi tumeanzia Arusha lakini tutafika mpaka mikoa mingine”
Alieleza Mgasa.
Kwa upande wake Afisa habari wa kampuni ya itel Fernando Wolle alisema wametoa msaada huo
kutokana na ushirikiano mzuri uliopo kati ya kampuni ya itel na jamii nzima ya
Kitanzania.
“Hatuwezi tukajisifu kwamba ni sisi tuliotoa msaada huu,
msaada huu unatokana na kuaminiana kati ya itel na Watanzania, kwa kifupi ni
kwamba kama ulishawahi kununua simu ya itel basi wewe ndiye uliyewezesha,
naomba tu Watanzania endeleeni kutumia simu zetu na kwa sasa tunayo itel S31,
ukinunua basi unaunga mkono jitihada hizi” Alisema Wolle.
Akieleza kuhusu msaada huo Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi
Uhuru Zurina Rajabu alisema kampuni ya itel haijakosea kutoa msaada huo katika
shule yake kutokana na uhitaji walionao.
“Tuna jumla ya wanafunzi wenye ulemavu wa akili 76, kwahiyo
itel hamjakosea kabisa kuja hapa Uhuru kutoa msaada huu, hawa watoto ni
binadamu kama walivyo wengine, na wengine tunawafundisha mpaka wanakuwa kawaida
na wangine waliomaliza wana maisha mazuri tu kwahiyo tunaomba ushirikiano
zaidi” Alisema Rajabu.
Shule ya msingi Uhuru ilianzishwa mwaka 1946 na mpaka sasa
ina wanfunzi zaidi 1500 na kati yao wanafunzi 76 wana ulemavu wa akili.
PICHA ZOTE ZA HAFLA HIYO ZIPO HAPA---
No comments:
Post a Comment