Thursday, August 31, 2017

RC. MAKONDA KUANZISHA KAMPENI YA KUCHANGIA UJENZI WA OFISI ZA WALIMU

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Poul Makonda ameanziasha rasmi kampeni ya kuchangia ujenzi wa nyumba za walimu katika jiji la Dar es salaam.

Akiongea katika mkutano na waandishi wa habari Mh. Makonda alisema kuwa mahitaji ya walimu ni zaidi ya ofisi 402 hiyo ni kwa walimu wa sekondari na shule za msingi.

Na ujenzi huo unatarajiwa kuanza tarehe 5 mwezi wa 9 na lengo la mkutano huu ni kuitambulisha kamati itakayosimamia zoezi hilo likiwa chini ya mwenyekiti wa kamati hiyo Canal Charles Mbuga akiwakilisha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

Katika ujenzi huo JKT imetoa vijana 300 watakao jitolea kujenga ofisi hizo pamoja na jeshi la Magereza wao wakiwa wametoa skari pamoja na Wafungwa watakao saidia kufyatua matofali pamoja na kujenga, bila kusahau Jeshi la Polisi pamoja Channel Ten watakao saidia kuitangaza kampeni hiyo.

Aidha Mh. Makonda alisisitiza kuwa bado mahitaji ni mengi na huu ni mwanzo tu hivyo wanaombwa wadau, wananchi na wapenda maendeleo kujitolea vitu kama Kokoto, Mchanga, Nondo, Cement, Mabati nk.

Pia wananchi wote wanaweza kuchangia huduma hiyo kwa benki ya CRDB akaunti namba 0150296180200 na mchango wao utakuwa umesaidia kujenge ofisi za walimu pamoja kuboresha elimu yetu kwani ukimuwezesha mwalimu utakuwa umeokoa wanafunzi ili waweze kupata elimu bora.

Na mwisho Mkuu wa Mkoa alipenda kuwashukuru wale wote waliowezesha hatua za awali kuweza kukamilika za kuanza kwa ujenzi huu na kwa baadi ya mashirika yaliyojitolea kwa dhati kama TBA pamoja NIC.

No comments: