Ikiwa zimebaki siku chache kabla ya kufanyika kwa tamasha
kubwa la jinsia linalotarajiwa kufanyika siku ya jumanne tarehe 5 mpaka 8 ya
mwezi wa 9 katika viwanja vya mtandao wa jinsia TGNP.
Maandalizi yakiwa bado yanaendelea kwa upande wa
wanaharakati wa semina za jinsia GDSS wameendelea kujipanga ipasavyo
kuhakikisha wanaonyesha vitu vikubwa Zaidi kwa kuwa wao ndio wenyeji wa tamasha
hili, na kusema kuwa hawatakubali kuja kufunikwa na wageni watakao kuja kwenye
tamasha hilo.
Afisa Program na nguvu za pamoja wa TGNP Bi. Anna Sangai akiendesha semina ya GDSS kwa kuchukua maoni na kuangalia nini kifanyike kwenye Tamasha la Jinsia ili lizidi kuwa zuri zaid kwa mwaka huu. |
Akiongoza semina hiyo afisa program wa nguvu ya pamoja Bi. Anna
Sangai alisema maandalizi yanaendelea vizuri na kwa mwaka huu tamasha hilo litachukua
Zaidi ya wanafunzi 150 wa shule za sekondari na msingi.
Miongoni mwa shule hizo ni shule ya msingi umoja na mabibo
sekondari zilizopo kata ya mabibo kwa idadi ya 25 msingi na 25 sekondari ambazo
zitakuja siku ya kwanza ambayo ni tarehe 5, na kundi la pili litakuwa kata ya
mwananyamara ambalo pia ni wanafunzi 50, 25 shule ya msingi mchangani na shule
ya sekondari makumbusho wanafunzi 25, na kundi la mwisho litakuwa shule ya
msingi kilimani wanafuzni 25 na kipunguni sekondari wanafunzi 25 hizi toka kata
ya kipunguni.
Aidha dada anna alipenda kuwasisitiza wanaGDSS kuwa wakarimu
kwa wageni wote lakini pia kuwa na upendo ili wageni wajione wako nyumbani na
kama ukiokota kitu cha mtu mwingine basi kipelekwe mahali husika ili kitangazwe
na kupewa mwenye kitu chake ili wageni wafurahie tamasha na kuona TGNP ni
sehemu nzuri na salama kwao.
Lakini sambamba na hilo wanaGDSS wametakiwa kuhakiki majina
yao ili waweze kujua wamapangwa vitengo gani vya kutoa huduma na pia kwa ajiri
ya kupewa vitendea kazi kama mabegi na Tshirt za tamasha hilo pamoja na huduma
nyinginezo kama chakula nk.
Na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa makamu wa kwanza wa rais
mwanamke kwa Tanzania mama samia suluhu hassani na kusema kuwa amashapelekewa
barua hivyo wanatarajia kama hatokuwa na shughuli nyingi za kiserikali
ataungana na jopo kubwa la wageni katika tamasha hilo.
baadhi ya washiriki wa semina ya GDSS ya wiki hii wakisikiliza kwa umakini muongozo unaotolewa na kiongozi wao. |
Bi. Heriet Kabende akichangia mada katika semina ya jinsia na maendeleo GDSS ilifanyika jumatano hii ikiwa semina ya mwisho kabla ya siku ya tamasha la jinsia linalotarajiwa kufanyika hivi karibuni. |
Bw. Innocent Siriwa akitoa maoni kuhusiana na Tamasha la Jinsia linalotarajiwa kuanzia jumanne ya tarehe 5 mpaka ijumaa 9 katika viwanja vya Mtandao wa Jinsia Mabibo jijini Dar es salaam |
Bi. Subira Kibiga akiendelea kuwafua wanafunzi wake kwa upande wa mashairi ili waweze kutoa kitu kizuri siku ya Tamasha la Jinsia linarotarajiwa kufanyika hivi karibuni. |
No comments:
Post a Comment