Tuesday, August 22, 2017

SUMAYE ALALAMIKA KUPOKONYWA MASHAMBA YAKE LA EKARI 326 NA EKARI 33 LILILOPO MABWEPANDE

Waziri Mkuu Mstaafu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Kanda ya Pwani Frederick Sumaye ameituhumu serikali ya Tanzania kwa kufanya maamuzi yasiyo zingatia sheria na katiba ya nchi kuhusu mgogoro wa mashamba ya familia yake na serikali.
Waziri mkuu Msataafu Mh. Fredrick Sumaye akiongea na waandishi wa habari kuhusu sakata lake la kudhurumiwa mashamba na wavamizi pamoja na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mapema leo kwenye ofisi za chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) kanda ya pwani.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Sumaye ameeleza kuwa licha ya mahakama kuu kuweka zuio la muda (court injuction) kuhusu mashamba mawili ya familia yake la Mabwepande jijini Dar es Salaam lenye ekari 33 linalomilikiwa na mtoto wa Sumaye ndugu Franklin Sumaye na lingine la MvomeroMkoani Morogoro lenye ekari 326 linalomilikiwa na mke wake Sumaye Esther Sumaye, serilaki imekaidi agizo hilo la mahakama na kulitwaa shamba hilo ili wavamizi waendelee kuishi maeneo hayo kinyume cha sheria, alieleza Sumaye.

Sumaye ameongeza kuwa hawezi kuchukua hatua yeyote kwasasa anasubiri maamuzi ya mahakama juu ya kesi hiyo ambayo bado inaendelea lakini ikitokea ameshindwa kesi hiyo atamuachia Mwenyezi Mungu.
"Mimi sing'ang'anii hayo mashamba ninachokiomba haki itendeke lakini serikali imeingilia majukumu ya mahakama na kulitwaa shamba wakati kesi inaendelea mahakamani hili jambo siyo sahihi kabisa kwa nchi yenye kufuata utawala bora" Alieleza Sumaye.

Sumaye amefunguka zaidi na kueleza kuwa serikali ikiendelea kufanya maamuzi bila kuzingatiia sheria itaendelea kulipa fidia na kuliingiza taifa katika hasara, kwasababu kesi zikienda mahakamani serikali lazima ishindwe.

No comments: