Ni sehemu ya msaada wa Tigo katika kuhakikisha upatikanaji wa maji safi na salama
Tabora, Agosti 22, 2017- Tigo Tanzania imejenga kisima cha maji chenye thamani ya Sh 18m/-katika kijiji cha Usongelani katika wilaya ya Urambo, mkoani Tabora kama sehemu ya ahadi iliyotolewa na kampuni hiyo ya kuunga mkono ya kuunga mkono ustawi wa kijamii katika maeneo inamohudimia pamoja na juhudi za kuunga mkono katika kuhakikisha kuwa wananchi wote nchini wanapata maji safi na salama.
Akizungumza kwenye sherehe ya makabidhiano iliyofanyika katika Kijiji cha Usongelani mkoani Tabora, Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa, Ally Maswanya alielezea matumaini yake kuwa kisima hicho kitachangia kwa kiwango kikubwa kupunguza tatizo la uhaba wa maji katika eneo hilo kwa kuipatia jumuia ya eneo hilo kupata maji ya uhakika, safi na salama.
"Tumejitahidi kuboresha maisha ya jamii , sio tu kwa kuhakikisha kuwa wanafurahia huduma nzuri za mawasiliano kutoka katika mtandao wetu, bali pia kupiga hatua zaidi kuhakikisha kuwa afya zao na ustawi wao unaboreka," alisema.
Maswanya alibainisha kwamba msaada huo unafanya vijiji vilivyonufaika kufikia 21, na hivyo kuwafanya watu zaidi ya 187,000 kunufaika na kujituma huko kwa Tigo katika kuwapatia watu maji safi na salama kote nchini.
Mwaka huu, Tigo inakusudia kuchimba visima katika maeneo yaliyo na uhitaji mkubwa ambapo inatarajiwa kuwa zaidi ya watu 350,000 watafaidika na mchango wetu wa kuisaidia juhudi za za kupunguza uhaba wa maji safi na salama uliopo nchini.
Makabidhiano hayo yalishuhudiwa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mheshimiwa Aggrey Mwanri ambaye wakati akiwashukuru Tigo kwa msaada unaohitajika sana alisema kuwa kisima hicho kitasaidia kwa kiwango kikubwa kuimarisha afya na ustawi wa jamii kwa kusaidia kukua kiuchumi na kijamii. Aliwataka watu wengine wenye mapenzi mema kujitokeza kuunga mkono jitihada za kuondokana na tatizo la uhaba wa maji katika mkoa huo.
Tunapenda kuwashukuru Tigo kwa kutusaidia katika jitihada zetu za kuwapatia maji ya uhakika katika eneo hili kwa kutatua uhaba wa maji uliokuwepo. Tunaamini kuwa upatikanaji wa maji safi na salama karibu na makazi kutaongeza pia uzalishaji wa kiuchumi hasa kwa wasichana na wanawake ambao hawatakuwa wakitumia tena muda mwingi kutafuta maji safi mahali pengine. Hii itawapa wasichana fursa ya kuhudhuria kwa uhuru shuleni na kuwapunguzia mzigo wa kijamii hasa wanawake, hivyo kupata nafasi ya kushughulikia kwa ufanisi majukumu yao ya kila siku kwa maendeleo ya taifa, " alisema Mkuu wa Mkoa.
No comments:
Post a Comment