Wednesday, September 6, 2017

VIDEO - ALICHOKISEMA ESTER BULAYA BAADA YA KUPEWA TUZO YA HESHIMA KWENYE TAMASHA...

               
Kufuatia kwa zoezi la ugawaji tuzo za heshima kwenye Tamasha la Jinsia mwaka 2017 ambalo lilitekelezwa na makamu wa kwanza wa Rais mwanamke nchini Mama Samia Suluhu Hassan, mbunge wa Bunda kupitia chama cha CHADEMA Mh. Ester Bulaya alikuwa ni miongoni mwa waliopewa tuzo hizo.


Mh. ester alipewa tuzo ya heshima kutokana na utendaji kazi wake lakini kubwa zaidi ni kuwa mwanamke mwenye uthubutu wa kugombea ubunge katika jimbo gumu zaidi la Bunda mkoani Mara ambalo halina historia ya kuongozwa na mwanamke na hivyo kuwafanya wanawake wengi kuliogopa, lakini Ester Bulaya alijaribu na kweli aliweza kushinda ubunge wa jimbo hilo.



Baada ya ushindi huo Ester Bulaya aliongea na Habari 24 na kuelezea ushindi wake na kutoa ujumbe kwa wanawake wenzake wanaopenda kuwa kama yeye.

                     

No comments: