Sunday, September 24, 2017

Mashabiki wataka kocha wa simba kutimuliwa.



Mashabiki kadhaa wamekuwa wakitaka uongozi wa Simba kufanya kila linalowezekana ili kumuondoa Kocha Mkuu wa Simba, Joseph Omog kwa kuwa wanaamini kikosi ni kikubwa kuliko yeye.

Sare ya mabao 2-2 dhidi ya Mbao FC, iliamsha mjadala mpya na mashabiki wameanza tena kutaka Mcameroon huyo aondoke.

Manara amesema, uongozi unapaswa kutafakari kila jambo kwa kuwa mwisho, kama ni sifa au lawama huenda kwa uongozi.

“Unajua mashabiki wanapaswa kujifunza na ikiwezekana kuwa watulivu na kuiacha taalum ifanye kazi. Mfano suala la sub linaweza kuwa limewaudhi, lakini hawajawahi kwenda mazoezini.

“Walimu ndiyo wanajua nani anafanya vizuri, nani wakimtumia kwa wakati gani itakuwa sahihi na si mashabiki wanamshabikia nani,” anasema.

“Lakini hiyo haitoshi, kila mmoja anakumbuka, sisi ndiyo tulikuwa tunaongoza kuwafukuza makocha na ikawa si kitu kizuri. Sasa hatuwezi kuwa kitu kidogo, kocha aondoke.

“Tunaweza kupata kocha mzuri kabisa na maarufu, lakini pia asipate matokeo tunayotaka. Hii nayo itaturudisha nyuma na kuongeza maneno tena, hivyo ni lazima kutafakari mambo na ikiwezekana kuangalia utatuzi sahihi wa tatizo. Kufukuza au kuajili si njia pekee ya kumaliza tatizo,” alisema.

No comments: