Mwenyekiti
wa Bodi ya Benki ya KCB Zuhura Muro akiongea na waandishi wa habari (hawamo
pichani) wakati wa hafla hiyo.
|
Raisi wa Shirikiso la Soka Tanzania (TFF) Wallace Karia
akiishukuru benki ya KCB Tanzania kwa udhamini huo.
|
Bodi ya Utendaji wa ligi kuu kwenye picha ya pamoja na Uongozi wa Benki ya KCB Tanzania na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF). |
Menejimenti
ya benki ya KCB Tanzania kwenye picha ya pamoja na Uongozi wa Shirikisho la
Soka Tanzania (TFF).
|
Uongozi wa
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwenye picha ya pamoja na Uongozi wa Benki ya
KCB Tanzania.
|
Benki ya KCB Tanzania leo imetangaza rasmi udhamini mwenza wa
ligi ya soka ya TFF Vodacom 2017/18 wenye thamani ya shilingi za kitanzania
325,000,000. Mkataba wa makubaliano hayo ulisainiwa rasmi leo na Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya KCB Cosmas Kimario na Raisi WA TFF Wallace Karia
-------------------------------------------------------------------------
Hafla hiyo ya makubaliano ilihudhuriwa pia na Mwenyekiti wa Bodi
ya Wakurugenzi, Benki ya KCB Tanzania, Bi, Zuhura Muro, Mwenyekiti wa bodi ya
Udhamini TFF, Mhe, Mohammed Abdulaziz,
Wakurugenzi wa Bodi ya KCB Tanzania, Wafanyakazi Benki ya KCB Tanzania,
wawakilishi wa vilabu vinavyoshiriki ligi kuu ya soka na waandishi wa habari.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kusainiwa mkataba huo,
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB Cosmas Kimario alisema kuwa udhamini huo
upo ndani ya vipaumbele vya benki kuleta
maendeleo katika sekta mbalimbali za kijamii ikiwemo michezo. “Sekta ya michezo ina mchango mkubwa katika kuleta maendeleo ya
kiuchumi na kijamii na pia ni chanzo cha ajira kwa vijana wengi nchini, hivyo
benki ya KCB imechukua uamuzi huu kujiunga na TFF kukuza mchezo wa mpira wa
miguu” alisema Kimario.
Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya KCB Tanzania Zuhuru Muro alisema
kuwa “Benki ya KCB Tanzania tunajivunia kuwa sehemu ya ligi hii na tunaamini kuwa
udhamini wetu utachangia kuleta hamasa kubwa kwa wapenzi wa mpira wa miguu na
kukuza vipaji vya vijana.” Alieleza kuwa udhamini huo utakuwa chachu ya
maendeleo kwa benki, wateja wake, TFF, wachezaji, mashabiki na wananchi kwa
ujumla.
Rais wa TFF aliishukuru benki ya
KCB kwa kuidhamini Ligi kuu Vodacom jambo ambalo alisema litasaidia kufanikisha
msimu huu wa ligi kuu 2017/18. Pia
alizitaka taasisi zingine na watu binafsi kuiga mfano huo kuweza kutoa
michango ya hali na mali ili kukuza maendeleo ya soka kwa timu za ligi kuu.
No comments:
Post a Comment