Leo ikiwa ni
siku ya tarehe 29 ya mwezi wa 9 sheikh mkuu wa dhehebu la khoja shia Tanzania Hemed
Jalala amezindua program ya ugawaji maji na vipeperushi bure iliyofanyika
katika msikiti wa kigogo jijini Dar es salaam.
Akiongea na
waandishi wa habari mapema leo msikitini hapo Sheikh Jalala amesema kuwa zoezi
hili la kugawa maji linaendana sambamba na kumuenzi Imam Hussein ambaye ni
mjukuu wa pili wa Mtukufu Mtume Mohamad ambaye alifariki kwa kuwatetea wanadamu
bila kuangalia itikadi zao za kidini, kikabila wala maumbile.
Sheikh Jalala
aliongezea kwa kusema kuwa imam hussein amekuwa ni alama kwa dunia kwa kukubali
yeye kufa ili watu wapate amani pamoja na kutendeana mema ikiwemo kupendana,
kuhurumiana kuheshimiana na alithubutu kuyafanya hayo wakati huo ambao mema
yalipungua katika dunia na hakukuwepo amani miongoni mwa wanadamu hao na
matokeo yake yalikuwa ni ugomvi na chuki ndani ya kizani hicho.
Maulana Sheikh Hemed Jalala akiongea na waandishi wa habari ambao hawapo pichani mara baada ya kuzindua programu ya kugawa maji na vipeperushi bure mapema leo jijini Dar es salaam |
Lakini leo
hii Imam Hussein anatufundisha watanzania kuwa ni watu wenye huruma, upendo
ushirikiano na amani tuliyopewa kama nuru yetu Watanzania, ndiyo maana msikiti
huu umeamua kuanzisha program kama hizi ikiwemo kuwatembelea wagonjwa,
kujitolea damu kwa hiari, kwenda kuwapa moyo wafungwa pamoja na kuwaona na
kuwapa misaada watoto yatima ikiwa ni miongoni mwa njia za kumuenzi Imam huyo
aliyejitoa kwa ajiri ya wanadamu.
Akiongezea Askofu
Mkuu wa kanisa la Tanzania Outreach Ministries Banza Suleiman amesema kuwa
kitendo kilichofanywa na msikiti huo ni chema na kinapaswa kuungwa mkono na
kila Mtanzania anaependa maendeleo kwani maisha yetu wanadamu yanategemea maji
kwa kiasi kikubwa, hivyo ili kumuunga mkono Rais Magufuli kufikia kuwa na
uchumi mzuri wa viwanda ni lazima watu wawe na maji ya kutosha ili waweze
kufanya kazi ipasavyo.
Askofu huyo
aliendelea kwa kusema kuwa mungu anambariki anaetoa hivyo kwa kujitolea huko
mungu atawabariki sana na hata serikali itafurahi kwa kuona hata tasisi za
kidini zipo kwa dhumuni la kuwajari wananchi wake kwa kuona kitendo
kilichofanywa na msikiti huo, lakini pia hata wananchi wataona ni jambo zuri
kwani maisha ya mwana damu yanategemea maji hivyo bila maji hakuna maisha.
Mwenyekiti wa Kata ya Kigogo Mbuyuni Bw. Hassan Nguogani akiongea na waandishi wa habari ambao hawapo pichani mapema leo jijini Dar es salaam. |
Na mwisho
Mwenyekiti wa Mtaa Kigogo Mbuyuni Bw. Hassan Nguogani alimalizia kwa kusema
wanaishukuru sana taasisi hiyo ya Shia kwani imechangia maendeleo ya kata hiyo
kwa kiasi kikubwa kwani hujitolea mambo mengi sana kama matibabu bure kwa
wagonjwa, husaidia watoto yatima katika kata hiyo ujitolea madaftari na vifaa
mbalimbali vya shule kwa wanafunzi na huduma nyingine nyingi.
Lakini pia
husaidia juhudi za kimaendeleo kama kupanda miti, kufanya usafi maeneo ya kata
hiyo na hata kuchangia ujenzi wa vitu mbalimbali katika kata hiyo, hivyo ufanya
majukumu mengi ambayo ni ya serikali lakini hujitolea wao na hivyo wakazi wa
kigogo hunufaika na nifahari sana kwa uwepo wa msikiti huo mahali hapo.
No comments:
Post a Comment