Baada ya kumalizika
kwa Tamsha la Jinsia lililodumu kwa siku 4 mfululizo kuanzia tarehe 5 mpaka 8
ya mwezi septemba katika viwanja vya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Mabibo jijini
Dar es salaam.
Afisa Program na nguvu za Pamoja Bi. Anna Sangai akitoa ufafanuzi wa jambo fulani katika Semina ya GDSS mapema jana jijin dar es salaam |
Washiriki wa
semina za jinsia maarufu kama GDSS zinazofanyika kila jumatano pamoja na
wafanyakazi wa mtandao huo wamekutana kwa pamoja wakiwa na lengo la kujadili
mapungufu au changamoto zilizotokea wakati wa Tamasha.
Akiongoza semina
hiyo Afisa Program na nguvu za pamoja Bi Anna Sangai alisema kuwa wakati wa
tamasha yalitokea mambo mengi kuna mazuri ambayo tunapaswa kupongezwa na kuna mapungufu
ambayo yanahitajika kurekebishwa ili yasitokee tena tamasha lijalo.
Bi. Neema Mwinyi akitoa maoni yake kuhusu mapungufu yaliyotokea kwenye Tamasha la mwaka huu mapema jana jijijni Dar es salaam |
Na pungufu
la kwanza ni kwa upande wa maegesho ya magari (parking) hayakuwa mazuri
kutokana kwamba hakukupangwa sehemu maalumu ya magari kwa mfano gari ya mgeni
ilitakuwa kuwe na sehemu iliyandaliwa kwa ajiri ya kukaa na wafanyakazi wa TGNP
pamoja na wageni waalikwa kulitakiwa kuwe na maeneo ya kukaa gari zao.
Ya pili ni
kwamba Mgeni Rasmi Mama Samia Suluhu Hassan hakutembelea mabanda ya
wajasiliamali alitembelea mabanda yaliyopo mwanzoni ambayo yalikuwa ya taasisi
kubwa kama LHRC, TAMWA, KIVULINI nk. Lakini
katika mabanda ya mbele ambayo yaliandaa vitu vizuri hakufika hivyo hajajua
wajasiriamali wamekuja na nini mwaka huu.
Bw. Innocent Siliyo akichangia mada katika mapungufu ya tamasha la jinsia 2017 |
Kwa usiku wa
mwafrika ulipendeza lakini watu hawakufuata utaratibu waliambiwa vazi la siku
hiyo ni vitenge, cha ajabu kila mtu alivaa anachokijua yeye hali ilyofanya kuwa
siyo tena usiku wa mwafrika wenye vazi maalum, na kingine watoa kuponi siku
hiyo walikuwa wakitoa kwa upendeleo hali iliyofanya baadhi ya wageni kukosa
kuponi.
Na changamoto
nyingine ni kukosekana kwa banda hata moja la kupima afya kama Angaza, Maria
stopes nk. Hali iliyowafanya watu wengi
kuulizia mahalali pa kupimia afya zao.
Baadhi ya wanaharakati walioshiriki semina ya GDSS iliyofanyika mapema jana makao makuu ya Mtandao wa Jinsia yaliyopo Mabibo jijini Dar es salaam |
Kwa upande
wa wana GDSS hawakuchangamkia fursa walipewa banda lakini halikuwa na kazi
nyingi za mikono za kushawishi wageni, hali iliyofanya wageni kutoka mikoani
kufanya vizuri katika Tamasha la mwaka huu na pia kutofahamu majukumu yao waliyopangiwa
na kufanya majukumu ya watu wengine.
Utaratibu haukuwa
mzuri kwenye upande wa ugawaji wa chakula kwani haikuwepo sehemu kwa wazee na watu
wenye Ulemavu hali iliyowafanya kupanga foleni kama watu wengine, lakini pia
kwa wagawa chakula ilikuwa ukimwambia namchukulia mzee au mlemavu wanakataa na
kumtaka aende kuchukua mwenyewe.
Na changamoto
ya mwisho ni ufungaji wa tamasha watu wengi walikuwa hawaamini kama kweli
limefungwa kwani siyo kama kama siku liliyofunguliwa ilikuwa gafla sana, hivyo
wadau wanaomba hata usiku wa mwafrika ungekuwa mwisho ili kuchangamsha ufungaji
wa tamasha hilo.
No comments:
Post a Comment