Mkuu wa
wilaya ya kinondoni mh. Ally Hapi jana amefanya ziara ya
kutembelea soko la makumbusho na kuongea na wafanya biashara pamoja na wakazi
wa maeneo ya karibu ili kufahamu changamoto zilizopo katika eneo hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Ally Hapi akitoa ufafanuzi wa jambo furani katika ziara yake iliyofanyika jana katika soko la Makumbusho jijini Dar es salaam. |
Katika mkutano huo wafanya biashara na wakazi wa kata ya makumbusho walipata nafasi ya kutoa kero zao na kuhoji mambo mbalimbali yakimaendeleo katika soko hilo na kupatiwa majibu ya papo kwa hapo na jopo alilokuja nalo mkuu wa wilaya huyo.
Mh. Hapi
ametoa agizo kwa meneja msimamizi wa mradi wa makumbusho ambae amemuwakilisha
muwekezaji kupeleka nyaraka zote za malipo waliyofanya katika ulipaji wa kodi,
na pia wamepewa muda wa mwezi mmoja tu kulipa deni lote wanalodaiwa na manispaa
ambalo ni zaidi ya million 70.
Meneja Msimamizi Mradi wa Makumbusho (Muwekezaji) Bw. Haidary Salumu akitoa ufafanuzi juu ya mashitaka yanayomkabili kuhusu kuwanyanyasa wafanya biashara wadogo wa eneo hilo |
Lakini pia
mkuu wa wilaya huyo ametoa agizo kwa jeshi la polisi kuweza kuwakamata
watuhumiwa wanne ambao ni Shabani,
Bonzo, Deo na Scorpion kwa makosa ya kuwaonea wafanya biashara wadogo wanauza
maji, pipi karanga, sigara katika kituo hicho kwa kuchukua bidhaa zao na kuwataka
watoe hela ndipo wapewe bidhaa zao.
Aidha mh.
Hapi aliendelea kusisitiza kuwa serikali ya awamu ya tano ipo kwa ajiri ya kuwakomboa
wanyonge hivyo haitakaa kimya kuona wananchi wake wanaonewa, hivyo kutoa agizo kwa
polisi kumkamata mtu anayeitwa Morel mkazi wa mbezi juu ambaye anasifika kwa
kudhurumu watu ardhi na wananchi kukosa kwa kushitaki kwa kuwa ni mtu mwenye
fedha.
Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kinondoni Bw. Abubakari Kunga akiendelea kutoa ufafanuzi juu ya elimu ya uraia na haki za wananchi. |
Na lingine
aliloagiza mkuu wa wilaya ni kusitishwa mara moja zoezi la ukusanyaji fedha kwa
pikipiki na boda boda ambalo lilikuwa likitekelezwa na muwekezaji huyo ambalo
limeonekana likiwaumiza wananchi hao kwa kutozwa fedha nyingi kinyume na
mkataba waliyokubaliana na manispaa ambao ndio waliowapa kibali hicho. Na kutoa
agizo ifikapo jumaa tatu apeleke nyaraka zote zinazoonyesha makusanyo
waliyokusanya toka mwanzo mpaka sasa na kutakiwa kuzilipa fedha hizo zote.
Lakini pia
muwekezaji huyo kuambiwa aache mara moja zoezi lake la kuweka walinzi katika
eneo hilo ambao wamekuwa wakiwaonea wafanya biashra wadogo na kusababisha
ugomvi na wizi katika eneo hilo kwani wakina shabani wakiwachukulia vitu
wanaenda kuviweka ofisini kwake, na kusisitiza kazi ya ulinzi na usalama ni ya
serikali na siyo ya muwekezaji.
Na mwisho
OCD wa kinondoni amepewa kazi na mkuu wa wilaya huyo ya kuhakikisha polisi
waliyotumika kuwakamata wafanyabiashara wadogo kwa kisingizio cha uzululaji na
kuwapeleka kituoni na kuwachaji fedha wachukuliwe hatua mara moja ya kufikishwa
mahakamani kusomewa mashitaka.
No comments:
Post a Comment