Saturday, October 28, 2017

RC MAKONDA ATEMBELEA MAENEO YALIYOATHIRIWA NA MAFURIKO JIJINI DAR ES SALAAM

Wakazi wa maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam wanaoishi maeneo ya karibu na mito pamoja na mabondeni wametakiwa kuacha tabia za kutupa taka taka, kuchimba mchanga na kuunganisha chemba za vyoo katika maeneo hayo.
Hayo yamesemwa mapema leo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Poul Makonda alipokuwa akitembelea maeneo mbalimbali ya jiji hilo yaliyoathiriwa na mvua kubwa zilizonyesha hivi karibuni.

Mkuu wa mkoa huyo alisema kuwa wananchi ni vema kuacha tabia hiyo kwani wanapotupa taka au kuchimba mchanga katika mito kwani hali hii inasababisha maji kukosa muelekeo hivyo kuingia katika makazi ya watu.
Lakini pia kwa chemba za choo zinapounganishwa katika mito hiyo inasababisha magonjwa ya mlipuko kama kipindu pindu na magonjwa mbalimbali ya matumbo.

Aidha Mh. Makonda alipenda kuwasihi wananchi wa maeneo hayo ya mabondeni kuishi kwa tahadhari kwani kama unahisi kwako si salama ni vema ungehama mapema kwani utabiri wa hali ya hewa unaonyesha kuanzia tarehe 1 ya mwezi ujao mvua itakuwa kubwa zaidi ya hii.
Lakini pia alisema kuwa kwa wilaya moja ya kinondoni peke yake zimebomoka nyumba zaidi ya 190 na nyingine zaidi ya 200 zimevamiwa na maji, hivyo kuwataka wnanchi wawe makini na hali hiyo kwani ni hatari kwa maisha yao.

Mkuu wa mkoa huyo alipokuwa akiongea na wananchi wa kawe alisema kuwa uhalibifu uliofanywa na maji na kuharibu daraja la Malichela, ameshaongea na jeshi la wananchi na karibuni unaanza ujenzi wa daraja la muda mfupi kipindi ambacho Tanroads wanajipanga kwa ajili ya kutengeneza daraja la muda mrefu.

Aliongezea kwa kusema kuwa zaidi ya billion moja zimetolewa na benki ya dunia kwa ajili ya mradi wakupasafisha na kurekebisha eneo la jangwani hivyo wapo katika mchakato wa kuelewana na Injinia na mpaka wiki ijayo kazi hiyo itaanza rasmi.

No comments: