Wanaharakati
wa semina za jinsia na maendeleo GDSS wamekutana mapema wiki hii lengo likiwa
ni kujadili faida na changamoto
mbalimbali za matumizi ya teknolojia ya habari na mwawasiliano (TEHAMA).
Akiongoza
semina hiyo muwezeshaji kutoka Mtandao wa jinsia(TGNP) Bi. Veronica Magayane alisema
kuwa wanaharakati wanajukumu kubwa la kuleta usawa na haki katika jamii hivyo
ni vema kutumia Tehama katika harakati zao na kujiletea maendeleo kama
wajasiliamali wadogo.
Wakitoa
maoni mbalimbali kuhusu matumizai ya Tehama wanaharakati hao walisema kuwa mfumo
wa elimu yetu siyo rafiki kwa matumizi ya Tehama kwani serikali ilitakiwa
kuweka mfumo huu kuanzia shule ya msingi na secondary ili wanafunzi waweze
kuelewa vizuri kitu hiki, na waweze kukitumia kwa faida yao ya sasa na baadae
na siyo kusubiri mpaka wafike chuo ndipo waanze kujifunza.
Lakini pia
ni kwa wazazi kukosa uelewa wa kutosha kuhusu teknolojia hii kwamba mzazi
anasema awezi kumnunulia kompyuta mtoto wake anaesoma kwa kudai hana fedha wakati
huo huo anachangia harusi zaidi ya laki mbili wakati ni kiwango ambacho unaweza
kuipata hiyo kompyuta, lakini pia kwa kuhisi atajifunza vitu vingi vibaya
ambavyo ni utamaduni wa nje ya taifa letu na kuhisi ataharibikiwa wakati
angefanya hivyo ingekuwa ni njia nzuri ya kumuandaa mtoto kufahamu Tehama ambayo
ingemsaidia kwa maisha yake ya baadae.
Na jambo
lingine wanaharakati walisema kuwa kwa watu wazima wengi wanahisi wao
hawastahili kutumia Tehama kwani ni mambo ya vijana wakati ni njia nzuri ambayo
ingewasaidia katika kutimiza majukumu yao na ingeweza kuwaletea faida katika
ujasiliamali wao kwani mtu unaweza kutumia Watsaap, ama Instagram kutangaza
biashara yako na ukapata wateja wengi kuliko kukaa sehemu moja kusubiri mteja
ambae hujui atakuja saa ngapi.
Aidha
wanaharakati waliendelea kusema kuwa njia hii endapo itatumiwa vibaya basi
inaweza kuleta matokeo mabaya katika biashara zao, mfano ukuwa unauza nguo na
ukapiga picha lakini ukaongezea rangi kupitia instagram mtu akihitaji nguo ile
ukampelekea inawezekana yeye alipenda ile rangi ilivyokolea lakini akaona
tofauti na uliyomletea itakuwa umempoteza mteja na atawaambia wengine hivyo hutapata
wateja tena watakao nunua bidhaa zako.
Lakini pia
mtu mwingine atakwambia amependa bidhaa yako na kwa kuwa umeweka na mwasiliano
atakupigia umpelekee hivyo katika hilo vingi hutokea unaweza kuvamiwa, kupigwa
na kuibiwa ulivyonavyo kama simu na hizo baidhaa ulizoendanazo kumpelekea mtu
huyo.
Na jambo
lingine kuna wale watu ambao wezi wa kurasa za watu(account/page) wanaweza
kuiba kurasa yako na kuitumia vibaya na wakati wewe ulikuwa ukiitumia kwa mambo
ya kibiashara tu, lakini wao wakaweka vitu vingine tofauti au wakaamua
kukuchafua wewe na biashara yako na hata muda mwingine kukutaka utoe pesa illi
waweze kukuachia kurasa yako ya biashara.
Lakini pia
wanaharakati wameshauri ili kuweza kupata maendeleo kupitia Tehama ni vyema
kutumia vizuri teknolojia hii kwa kutoa taarifa za ukweli ili unachokitangaza
kiendane kweli na ubora wa bidhaa yako ili kujitengenezea mazingira mazuri kwa
wateja wako.
Serikali kwa
kushirikiana na vikundi vya wanaharakati
kama GDSS kusaidia kusambaza elimu hii
ya matumizi bora ya Tehama na kwa kiasi gani inaweza kutumiwa na
wajasiliamali ili kujiletea maendeleo wao na vizazi vya vya sasa na vijavyo.
No comments:
Post a Comment