Aliyekuwa mgombea urais 2015 kupitia ACT - Wazalendo Mama Anna Mghwira ambaye kwa sasa ni mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, ametangaza rasmi kujiunga na chama cha Mapinduzi CCM.
Tukio hilo limetokea leo mjini Dodoma kwenye uzinduzi wa mkutano wa Umoja wa Wanawake Tanzania wa CCM (UWT), ambao umehudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Katika mkutano huo mama Anna Mghwira amesema ameamua kufanya hivyo baada ya kuona jitihada za CCM katika kuleta maendeleo, hivyo akaona ni vyema akajiunga nao.
"Mimi baada ya kuwa Mkuu wa Mkoa kwa muda mfupi nimeona mengi ndani ya CCM na nimeona sio mbaya nikitamka kuwa naungana nanyi rasmi, ahsanteni sana kwa kunipokea na kama niliposikia hotuba ya Mwenyekiti ni kweli kuwa sisi akina mama ndiyo wenye jukumu la kubeba nchi. Na mimi naungana na akina mama wenzangu wa UWT wenye malengo ya kuendeleza taifa", amesema mama Anna Mghwira.
Mama Anna Mghwira anakuwa kiongozi mkubwa wa tatu kitaifa wa ACT Wazalendo kujiunga na CCM ndani ya mwaka huu.
No comments:
Post a Comment