Vijana ni
jeshi kubwa ambalo likipewa nafasi na kutengenezwa vizuri litaweza kuleta mabadiliko
na utetezi mzuri wa haki za binadamu hapa nchini kwetu na duniani kwa ujumla.
Hayo yamesemwa
na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sharia na Haki za Binadamu Bi. Helen Kijobisimba
mapema jana katika maadhimisho ya siku ya haki za binadamu kimataifa.
Maadhimisho hayo
ambayo ufanyika kila mwaka kila ifikapo tarehe 10 ya mwezi disemba na yalianza
kuadhimishwa toka mwaka 1950 pale tu lilipotoka tamko la la Umoja wa Mataifa kuhusu
siku hiyo mwaka 1948.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Bi. Helen Kijobisimba akiongea na waandishi wa habari mapema jana Karim jee jijini Dar ese salaam |
Mkurugenzi huyo
alisema kuwa wao wameamua kuadhimisha kwa siku ya ijumaa tarehe 8 kutokana
kwamba jumaa pili itakuwa ni siku ya ibada na pia serikali itakuwa na
maadhimisho yake hivyo wao wakaona ni vyema kufanya siku hii.
Aidha mkurugenzi
huyo alisema kuwa Lengo kuu la maadhimisho hayo ni wao kama watetezi wa haki za
binadamu kujipima katika utetezi wa haki hizo, wamefikia wapi na wanahitajika
nini wafanye ili kuweza kufika pale panapostahili kufikiwa katika mawswala ya
haki ndani ya taifa.
Lakini pia
kujua wamefanikiwa kiasi gani kuishauri serikali kutekeleza upatikanaji wa haki
za binadamu kwa kuwa wao ndio watekelezaji wakubwa kama walivyokubali kusaini
mikataba ya kimataifa ya kutetea na kulinda haki hizo.
Kwa mwaka
huu maadhimisho hayo yamebeba ujumbe unaosema “haki za bianadamu na viwanda”
Baadhi ya washiriki wa maadhimisho ya siku ya Haki za Binadamu yaliyofanyika mapema jana jijini Dar es salaam. |
Na hii ni
kwa nchi yetu kuelekea uchumi wa viwanda je? haki za binadamu zitaweza kufuatwa
na kulindwa katika maeneo hayo, lakini pia kwenye viwanda kutazalisha vitu kama
ajira, biashara na shughuli nyingine, sasa katika maeneo hayo wasimamizi na
wafanyakazi wataweza kuzitetea na kuzilinda haki za binadamu.
Bi Helen aliendelea
kusema kuwa licha ya kuangazia katika maeneo ya viwanda lakini wamejadili haki
mbalimbali kama haki ha kuishi, haki ya kulindwa, uhuru wa vyombo vya habari,
uhuru wa kujieleza na haki nyinginezo.
Na pia
kuendelea kupinga vitendo vya watu kutekwa na kupotea kama Benny Sanane,
mwandhishi wa habari wa Mwananchina ndugu. Azory na wengineo lakini pia kujaribu kumuua Mbunge
wa Singida Mashariki Mh. Tundu Lissu na mengine mengi yanayoendelea.
Kwa upande
wake mwenyekiti wa tume ya Haki za Binadamu ya Utawala Bora Bw. Bahame Tom Nyanduga
amevitaka vyombo vya usalama ikiwa ni jeshi la polisi pamoja na mahakama
kutekeleza majukumu yao kama inavyotakiwa ili kuwezesha haki kupatikana.
Aliendelea kusema
kuwa vyombo hivi vinatakiwa kuhakikisha chunguzi zinafanyika kwa muda mfupi na
stahiki na pia kesi zisizungushwe sana ili kuweza kurahisisha upatikanaji wa
haki kwa raia.
Lakini pia
alisema kuwa serikali ina jukumu kubwa la kuhakikisha kuwa haki za binadamu
hazivunjwi kwani wao wamesaini mikataba ya kimataifa na ya kikanda hivyo ikishindwa kuzuia matukio kama
yanayotokea sasa ya watu kukwa na wengine kuuwawa hii inasababisha kuonekana
kuwa imeshindwa kutekeleza mikataba iliyoingia.
Na mwisho
alisema kuwa wao kama tume ya haki za binadamu na utawala bora jukumu lao ni
kuishauri serikali kuhusu maswala yanayohusu haki za binadamu na kuhakikisha
haki hizo hazivunjwi katika nchi yetu.
No comments:
Post a Comment