Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikagua Kitalu Nyumba (Green House) katika ziara yake ya kikazi alipotembelea Chuo cha Kilimo Mtwara Kilichopo katika kijiji ch a Naliendele katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Mjini, Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha Kilimo Mtwara Ndg Elias L. Maijo, Juzi 22 Disemba 2017. Picha Zote Na Mathias Canal
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikagua mashamba mbalimbali ya uzalishaji wa mazao ya kilimo katika ziara yake ya kikazi alipotembelea Chuo cha Kilimo Mtwara Kilichopo katika kijiji cha Naliendele katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Mjini, Juzi 22 Disemba 2017.
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akizungumza na Wakuu wa Idara na Wafanyakazi wa Chuo cha Kilimo (MATI) Mtwara Kilichopo katika kijiji cha Naliendele katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Mjini, Juzi 22 Disemba 2017.
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo mara baada ya kukagua mashamba mbalimbali ya uzalishaji wa mazao ya kilimo katika ziara yake ya kikazi alipotembelea Chuo cha Kilimo Mtwara Kilichopo katika kijiji cha Naliendele katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Mjini, Juzi 22 Disemba 2017.
Na Mathias Canal, Mtwara
Wakufunzi wa Vyuo vya Kilimo kote nchini wametakiwa kutofanya
kazi kwa mazoea badala yake kufanya kazi kwa Weledi, Ubunifu na Maarifa ili
kuongeza tija katika majukumu yao ya kufundisha wanafunzi ambapo baadae
wanazalisha wataalamu mbalimbali katika sekta ya Kilimo.
Kauli hiyo imetolewa juzi 22 Disemba 2017 na Naibu Waziri wa
Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa wakati akizungumza na Wakuu wa Idara na
Wafanyakazi wa Chuo cha Kilimo (MATI) Kilichopo katika kijiji cha Naliendele katika
Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Mjini.
Alisema kuwa watendaji hao wanapaswa kuwa wabunifu katika nyanja mbalimbali zitakazowawezesha kuwa na kipato cha ziada kwa kufuata sheria,
taratibu na kanuni.
Alisema kuwa kufanya hivyo kutawanufaisha kuwa na kipato
kitakachowawezesha kuendesha chuo pasina kutegemea serikali kwa kina jambo ambalo litapunguza malalamiko dhidi ya serikali kufanya kila kitu.
Aidha, alisisitiza viongozi wa vyuo vyote vya Kilimo nchini
kutumia vyombo mbalimbali vya Habari sambamba na mitandao ya kijamii ili
kutangaza maudhui ya vyuo na kozi zinazofundishwa ili kurahisisha wanafunzi
kupata wepesi katika uchaguzi wa vyuo vya kusoma.
Katika ziara hiyo Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa
alitembelea na kujionea miundombinu ya Taasisi na kazi za mafunzo ikiwa ni
pamoja na kuangalia shughuli za uzalishaji wa mazao mbalimbali.
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Chuo cha Kilimo Mtwara Ndg Elias L. Maijo alimpongeza Naibu Waziri huyo wa Wizara ya Kilimo kwa
kuaminiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe
Magufuli na hatimaye kuteuliwa kumsaidia katika majukumu yake ambapo pia ameahidi
kutekeleza maelekezo yote yaliyotolewa.
No comments:
Post a Comment