Mwakilishi wa QNET Tanzania, Benjamin Mariki akikabidhi vyakula kwa mlezi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Khayraat Orphans Centre kilichopo Kigogo Kati, Bi. Khadija Hussein jana. |
Moja kati ya
taasisi inayokua kwa kasi sana Tanzania ya masoko ya mtandao QNET, leo imetoa
msaada wa mashine yenye mfumo wa kusafisha maji ya Water purifier na chakula
chenye thamani ya zaidi ya Tsh milioni 2 kwa kituo cha watoto yatima cha
Khayraat jijini Dar es salaam.
Msaada wa QNET ni sehemu
ya juhudi za kampuni hiyo za kuwajibika katika jamii, ambazo zimeelekezwa
katika kutoa msaada wa upatikanaji wa maji safi na salama kwa zaidi ya watoto
500 wenye uhitaji katika kituo cha kulelea watoto yatima na kuwapatia chakula kwaajili
ya kuwawezesha kufurahia sikukuu za krimasi katika kipindi hiki cha sikukuu
kama watoto wengine.
Kwa mujibu wa mwakilishi
wa QNET Tanzania Benjamin Mariki, kampuni ya mauzo ya moja kwa moja ina sera
bora ya uwajibikaji kwa jamii ambayo inatafuta kutoa kwa jamii inayoihudumia.
“Katika kampuni ya QNET,
tunaamini kuwa zaidi ya kusambaza bidhaa zenye ubora wa kiwango cha juu kwa
wateja wetu, tuna jukumu la kusaidia serikali na wadau wengine katika
kutekeleza shughuli ambazo zina athari nzuri kwa jamii, hasa miongoni mwa
wanajamii wenye uwezo mdogo,” alisema Mariki.
Mariki alisema kuwa
msaada uliotolewa kwaajili ya kituo ni pamoja na ufungaji wa mashine ya
kusafishia maji, kilo 100 za Mchele, kilo 100 za maharage, kilo 100 za unga,
lita 60 za mafuta ya kupikia, kilo 100 za sukari, kilo 100 za sabuni ya kufulia
pamoja na biskuti, pipi na juisi.
Akipokea msaada huo,
Mwasisi wa kituo cha Khayraat Orphans Centre, Bi Khadija Khussein aliishukuru
kampuni ya QNET kwa kutoa msaada akisema kuwa msaada huo utawasaidia kwa
kiwango kikubwa watoto walioko kituoni.
“Tunashukuru kwa msaada
huo tukiwa tunatambua kuwa mashine ya kusafishia maji ya water purifier
itasaidia katika kurahisisha upatikanaji wa maji safi na salama kwaajili ya
watoto, hivyo kutoa uhakika wa afya kwa watoto kwa kuzuia magonjwa yanayoambukizwa
kwa maji kama vile typhoid na Kipindupindu wakati vyakula vitawapa watoto nafasi
ya kufurahia sikukuu ya krimasi na mwaka mpya”. Alibainisha Bi Khussein
No comments:
Post a Comment