Na Ramadhani Kangale
Waislam Nchini wametakiwa kutoa ushirikiano pale wanapofika wafadhili
wakujenga misikiti katika maeneo yao ili kuendeleza mbele uislamu,
Wito huo umetolewa jijini Dar es Salaam na muakilishi wa Taasisi ya Human Relief Fondation ya
nchin Bahrain hapa Tanzania Mbarak Fahmy
wakati wa ziara waliyoifanya viongozi wa taasisi hiyo kutembelea miradi yao ya
misikiti waliyo ijenga hapa tanzania.
Fahmy alisema kuwa endepo kutakuwepo
ushirikiano wa kutosha baina ya waumini
na wafadhili wanaojenga misikiti itakuwa rahis wafadhili kutekeleza majukumu
yao bila kujali umbali wa eneo lilo hitajika kujenga misikiti au madrasa.
Akifafanua ushiriiano huo ni kutoa maeneo alisema kuna baadhi ya waumini
wadini hiyo wamekua wakimiliki maeneo makubwa lakini kutoa kwa ajili ya ALLAH
anaonatabu huku akilazimika kutembea umbali mrefu kwenda kufanya ibada.
Akizungumzia malengo ya taasisi hiyo kwa hapa Tanzania wanakusudia kujenga
kituo kikubwa cha watoto yatima hapa tanzania maeneo ya chanika na kigamboni
pamoja na huduma zote za kijamii ikiwemo uchimbaji wa visima na ujenzi wa
misikiti na madrasa.
Aidha alisema lengo la kujenga kituo cha watoto yatima ni kuwaokoa watoto
hao wasiingie katika makundi ambayo yasiyofaa na ni hatarishi amesema kumekuwa
na wimbi la watoto wa mitaani wengi wao
wamepoteza wazazi wao na wengine kutelekezwa na wazazi au walezi hivo inakua
aipendezi kuachwa wakizurula mitaani nilazima wachukulliwe wapewe elimu ili
nawao waje kuwa watu wema na kujitambua nakua na familia zao katika kuliona
hilo ndipo walipoweka mikakati ya kutaka kuanzisha vituo hivo
Misikiti waliyotembelea viomgozi hao ni msikiti Li-lahi uliyopo mbezi
malamba mawili wilayani ubungo na msikiti wa AL-akswa uliyopo Zingiziwa chanika
wilaya ya Ilala na kuwagawiwa sadaka ya nyama ya Ng'ombe
No comments:
Post a Comment