Na.
Atley Kuni – OR TAMISEMI Dodoma
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli, ameweka jiwe
la msingi kwenye jengo la Ghorofa nne la
Ofisi za Taifa za Takwimu zilizopo
Mkoani Dodoma huku akionya vikali watu
wanao potosha takwimu na kuwatisha watanzania.
Rais
Magufuli amesema, wapo watu kwa Makusudi kabisa wamekuwa wakiupotosha umma juu
usahihi wa takwimu mbali mbali za nchi bila kuwa na vyanzo sahihi vya takwimu
ambao ni Ofisi ya Taifa ya Takwimu.
“Mmesikia
wenyewe hapa tumekuwa namba mbili kwa ubora wa takwimu katika nchi za Afrika,
tukitanguliwa na Nchi ya Afrika Kusini, ametuambia mkurugenzi mkuu wa Takwimu
Mama Chuwa, lakini wapo watu wengine sijui takwimu zao wanazitoa wapi na kuwadanganya
wananchi” amesema Mh. Rais
Rais
Magufuli ameiagiza Ofisi ya Taifa ya takwimu, kuitumia ipasavyo sheria ya
takwimu namba 37 ya mwaka 2015 kifungu kupitia kifungu kidogo cha 3 hadi cha 5
ambacho kinawalenga wapotoshaji wa takwimu na kwakutumia kifungu hicho basi mtu
anaweza kufungwa kati ya miezi sita hadi miaka mitatu au faini ya kati ya Mil.
Moja hadi 10 au vyote kwa pamoja.
Awali
akisoma taarifa ya maendeleo ya taarifa ya takwimu Mkurugenzi mkuu wa Bodi ya
Taifa ya Takwimu Nchini Dkt. Albina Chuwa, alisema mpango uliopo mbele yao ni
uboreshaji wa majengo, kusomesha wataalam, lakini pamoja na kuweka viwango bora
vya ukokotoaji wa takwimu.
“Mhe.
Rais tunajenga Jengo la Ghorofa moja pale mkoani Kigoma, nikuhakikishie kupitia
wadau wetu wa maendeleo jengo hilo tutalikamilisha bila kuhitaji msaada wa
serikali” alisema Dkt. Chuwa.
Chuwa
amesema, mbali na kuendesha sensa ya taifa tangu mwaka 1967 wakati wa
watanzania walipokuwa Mil. 13, Ofisi yao pia imeendelea na zoezi la sensa ya
watu na makaazi kwa miaka tofauti na mwaka wa mwisho kufanya sensa 2012
watanzania walikuwa Mil. 45, huku akitoa makadiri ya watu Mil. 60 na zaidi
ifikapo wakati wa Sensa ya 2022
Awali
kabla yakumkaribisha Mh. Rais, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango,
alimwambia Mh. Rais kuwa wanawashukuru sana wadau wa maendeleo kwa jinsi
wanavyozidi kushirikiana na Nchi ya Tanzania katika shughuli za maendeleo
hasa Benki ya Dunia.
“Mhe.
Rais kazi kubwa unayoifanya, wenzetu (World Bank) na wadau wengine wa Maendeleo
wanaithamini sana na ndio maana wamekuwa bega kwa bega katika shughuli za
Maendeleo alisema Mpango na kuongeza kuwa jengo linalojengwa Dodoma ni la pili,
jengo la kwanza lipo Zanzibar na linategemewa kuzinduliwa mapema mwaka ujao.
Kwa
upande wake Yasin Ringo Mtaalam wa ujenzi alimwambia Mh. Rais Jengo linalojengwa
Mjini Dodoma, hadi kukamilika kwake litatumia Bil. 11.7
Akihitimisha
Hotuba yake Mhe. Rais amezitaka taasisi zote nchini kutoa ushirikiano wa
kutosha kwa Bodi ya Taifa ya Takwimu ili kazi wanayoifanya iwe na ufanisi, huku
akimuagiza Waziri wa Fedha kufatilia suala la Airtel kwani inaonesha kampuni
hiyo ilikuwa mali ya TTCL.
Mbali
na kufanya shughuli ya uwekaji wa jiwe la Msingi Mh. Rais hakusita kuongelea
mambo mbali mbali yanayo husu uchumi wa nchi na kusema kuwa uchumi wa nchi
umekuwa kwa kiwango cha aslimia 6.8 huku mfumuko wa bei ukishuka na kufikia
asilimia 4.4 ambapo Tanzania imeongoza katika ukanda wa nchi za Afrika
Mashariki kwa kuwa na uchumi unaokuwa vizuri na kuwa miongoni mwa Nchi 5
zinazofanya vizuri barani Afrika katika suala la Ukuwaji wa Uchumi.
No comments:
Post a Comment