Tofauti na taarifa zilizochapishwa zinadozai
kuwa Tigo ndio mtandao wenye gharama kubwa zaidi, Tigo ingependa kuwataarifu
kuwa wateja wetu wanafurahia mojawapo ya gharama nafuu zaidi nchini.
Bando zetu zinaanzia TZS 500; hakika wateja
wa Tigo wanaonunua bando ya sauti ya TZS 500 kupitia menu yetu mpya ya 147*00 wanapata
dakika 16. Pamoja na hili, wateja wa Tigo wanaonunua bando hii wanapokea bonasi
ya dakika tano (5) BURE kila mara wanaponunua bando hii kupitia promosheni ya TUMEKUSOMA
ambayo inawapa jumla ya dakika 21. Kwa hiyo kwa bando la TZS 500, bei zinaweza
kufikia TZS 17.2 kwa dakika bila kujumuisha kodi.
Bando
ya TZS 1000 inayonunuliwa kupitia *147*00#
inawapa wateja wetu dakika 55, ambapo pia wanapokea bonasi ya dakika 30 BURE
kupitia promosheni ya TUMEKUSOMA. Hii inawapa jumla ya dakika 85; kwa hiyo bei
inaweza kufikia TZS 8.5 kwa dakika bila
kujumuisha kodi.
Tigo
inajulikana kwa promosheni kabambe na ubunifu wa ofa. Tigo pia imejijengea jina
kama mtandao unaowaelewa zaidi wateja wake na kuwapa bidhaa zinazoendana na
mahitaji ya soko.
Wateja wa Tigo ndio watumiaji wa simu pekee
wanaopokea bonasi za bure kwa kila bando wanayonunua, hivyo kuhakikisha kuwa
wateja wa Tigo wanafurahia huduma bora zaidi kwa viwango bora na nafuu nchini.
Kupitia
huduma zake za kipekee za sauti, ujumbe mfupi, intaneti yenye kasi ya juu ya 4G
na huduma za kifedha kupitia simu za mikononi, Tigo inaongoza kwa ubunifu wa
kidigitali ikiwemo;
- Tigo Halichachi ndio bando ya kwanza
iliyowezesha wateja wa simu nchini kutumia bando zao za simu bila muda wa
ukomo wa matumizi.
- Kuwa kampuni ya kwanza ya simu kuzindua
simu za Smartphone zenye lugha ya Kiswahili
- Kuwa kampuni ya kwanza ya simu kuzindua
Facebook ya bure kwa lugha ya Kiswahili
- Kampuni ya kwanza ya simu kuzindua
huduma za fedha kupita smart apps
- Huduma ya kwanza yenye uwezo wa
kubadili thamani ya fedha kwa sarafu ya nchi husika Afrika Mashariki iliyowezesha
wateja kufanya miamala ya uhakika ya fedha kupitia simu za mkononi kwenda
nje ya nchi.
Tigo
pia inajivunia mtandao mpana, wa uhakika zaidi wa 4G nchini, uliosambaa katika
miji 24 Tanzania, hivyo kuwawezesha wateja kufurahia maisha ya kidigitali.
No comments:
Post a Comment