Marekani imefeli
kuulazimisha ulimwengu kukubaliana na azimio lake lililokinyume na
sheria, wakati mkutano mkuu wa Umoja wa
Mataifa ulipopitisha kwa idadi kubwa ya wanachama wake,kupinga azimio la Trump linaloitambua
Jerusalem kama Mji Mkuu wa Israeli.
Pamoja na vitisho vya Marekani kwa nchi za dunia kuwa
itainyima misaada ya kifedha, kupitia Mwakilishi wake katika Umoja huo wa
Mataifa kwamba “Aidha fedha au kulipitisha azimio”, Marekani na Israeli pamoja
na nguvu zao hazikuweza isipokuwa
kuzikinaisha nchi 7 tu, katika kupigia kura ya hapana azimio hilo zikiwemo
zenyewe.
Nchi 128 zimelipigia kura ya ndio azimio hilo,ambazo ni sawa
na watu bilioni 7 walio ulimwenguni, sawa na asilimia zaidi ya 90% ya wakazi wote, huku azimio hilo
likiwa linalazimisha kuwa kwake, kwa kupata zaidi ya theluthi mbili ya wajumbe
wakamati kuu ya mkutano mkuu, likiwa na uzito sawa na maazimio ya Baraza la
Usalama.
Tanzania vilevile imepigia kura ya ndio azimio hilo ikiwa
pamoja na nchi nyingi duniani, zikiwemo China, India, Urusi, Uingereza, Ufaransa,
Ujerumani na idadi kubwa ya nchi za Umoja wa Ulaya, nchi zote za kiislamu na
kiarabu pia nchi nyingi za Amerika ya
Kusini.
Kilichoshangaza zaidi ni kuona dola ya Vatikani imepinga
azimio la Trump, dola ambayo yenyewe
inawakilisha ulimwengu wa kikristo, huku yakiwa makubaliano ya kiislamu,
kikristo na kibinaadamu yote yanapinga azimio la Trump lisilo la kisheria na si
la kiuadilifu, ambalo pia linakwenda kinyume na kanuni na sheria zote za
kimataifa.
No comments:
Post a Comment