Wateja watatu
wajishindia TSH 15 milioni, 10 milioni na 5 milioni!
Wengine
150 wajinyakulia zawadi za TSH 1 milioni na 500,000 kila mmoja!
Dar es Salaam, 31 Desemba,
2017
‘Nimeanza mwaka mpya nikiwa milionea!’ alisema
Lugano Thomas Mlini, ambaye ni dereva na mkaazi wa Mbezi Makonde, jijini Dar es
Salaam alipotaarifiwa kuwa amejishindia shilingi milioni 15 kutoka Tigo.
Kupitia huduma yake ya Tigo
Pesa, kampuni ya simu inayoongoza ya Tigo imewageuza Watanzania watatu kuwa
matajiri wapya kwa mwaka 2018.
‘Ndoto zangu za kuanzisha
biashara sasa zimetimia! Ahsanteni sana Tigo’ alisema Kulthum Salim Ally,
mkulima na mkaazi wa Tunduru, Ruvuma ambaye naye alijinyakulia kitita cha
shilinigi 10 milioni katika drooo kabambe ya promosheni ya Tumia Tigo Pesa na
Ushinde iliyofanyika siku ya mkesha wa kuamkia mwaka mpya, katika ofisi ya
makao makuu ya Tigo jijijni Dar es Salaam.
‘Nilienda kulala nikiwa
maskini na sasa nimeamka nikiwa tajiri’ alisema Mariam Josef maligisa, Mkulima
na mkaazi wa Nagangu, Lindi aliyeamka kutoka usingizini ili kupokea simu yake
na kutaarifiwa kuwa naye amejishindia TSH 5 milioni kutoka Tigo.
Akitangaza washindi katika
droo hiyo ya kuukaribisha mwaka mpya, Meneja wa Wateja wa Tigo Pesa, Mary Rutta
alisema, ‘Tigo pesa ni zaidi ya huduma ya kufanya malipo. Ni sehemu ya maisha.
Kwa hiyo leo tumewawezesha wateja wetu kutumiza ndoto zao za msimu wa sikukuu
na Mwaka Mpya kupitia huduma ya Tigo Pesa.
Alibainisha kuwa Tigo
imetoa jumla ya shilingi 120 milioni kwa watu 153 kutoka maeneo mbali mbali ya
nchi. Wateja walishinda zawadi nono za kila siku baada ya kutumia huduma ya
Tigo Pesa.
‘Pia tunajivunia mchango
wetu katika kufanikisha upatikanaji wa huduma za kifedha nchini. Kupitia Tigo
Pesa, tunawawezesha mamilioni ya Watanzania kutuma na kupokea zaidi ya TSH 1.7
bilioni kila mwezi. Hii inawawezesha wateja wenyewe pamoja na jamii, huku
ikichangia ukuaji wa uchumi wa nchi,’ aliongeza.
Kwa upande wake, Kaimu
Mkurugenzi wa Huduma za Masoko wa Tigo, Willima Mpinga alisema kuwa,’Tigo
inawatakia Watanzania wote Mwaka Mpya wenye furaha na mafanikio. Tigo ni
mtandao unaowaelewa zaidi wateja na kujibu mahitaji ya soko. Tulizindua
promosheni ya Tumia Tigo Pesa na Ushinde kwa dhumuni kuu la kuwawezesha wateja
wetu kushinda pesa zitakazowawezesha kutimiza malengo yao ya mwisho mwaka.’
Tigo Pesa ni huduma ya
kifedha kwa njia ya simu ya pili kwa ukubwa nchini. Tigo Pesa ina mtandao
mpana zaidi wa wakala na watoa huduma zaidi ya 70,000 waliosambaa nchini kote.
Tigo Pesa pia ilikuwa ndio huduma ya kwanza Afrika Mashariki iliyowezesha
wateja kutuma fedha kwenda nchi nyingine kwa kutumia viwango na fedha za nchi
husika.
Tigo ndio kampuni
inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali ikijivunia huduma bora za sauti, SMS,
intaneti yenye kasi ya juu zaidi ya 4G iliyosambaa katika miji 24 nchini,
pamoja na huduma za kifedha. Mtandao wa Tigo pia ni maarufu kwa promosheni na
ofa zake bunifu kwa wateja.
Tigo ilianza kutoa huduma
zake Tanzania mwaka 1995 na kwa miaka mitatu sasa ndio kampuni ya simu inayokua
kwa kasi zaidi nchini. Kwa sasa Tigo ndio kampuni ya simu ya pili kwa ukubwa
nchini ikiwa na wateja zaidi ya 11.6 milioni.
|
Friday, January 5, 2018
Tigo Yapata Mamilionea Wapya wa Mwaka Mpya 2018
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment