Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya FINCA Tanzania, Issa Ngwegwe akizungumza kwenye Kongamano la huduma jumuishi za kifedha wenye lengo la kukuza upatikanaji wa huduma hizo leo jijini Dare Es Salaam. |
Mkurugenzi Mtendaji FINCA Canada, Ms.Stephanie Emond akizungumza kwenye kongamano |
Mkurugenzi Uendeshaji wa FSDT Irene Majede akielezea jambo kwenye kongamano la Huduma Jumuishi za Kifedha leo.
|
Wadau wakifuatilia jambo |
Benki ya kutoa mikopo
midogo midogo inayoongoza Tanzania FINCA Micro-Finance Bank, kwa kushirikiana
na MasterCard Foundation, taasisi ya kimataifa ambayo inatoa ushirikishaji wa
kifedha na kuendeleza elimu kwa vijana barani Africa, leo imefanya mkutano wa
siku moja wa Ushirikishaji wa Kifedha jijini Dar es Salaam wenye lengo la
kushirikishana ujuzi miongoni mwa wadau mbalimbali katika kupanua upatikanaji
wa huduma za kifedha kupitia katika mifumo mbalimbali ya kidigitali.
Mkutano huo, ulilenga kutathmini
mafunzo yaliyotolewa kwa miaka mitano ya ushirika baina ya FINCA na Mastercard
Foundation kwa lengo la kukuza huduma za kifedha kwa jamii ya watu walio katika
sekta isiyo rasmi katika nchi za Tanzania, Zambia na Malawi kupitia matumizi ya
teknolojia za kisasa.
Mkutano huo ulihudhuriwa na watoa
huduna za kifedha, wafadhili, watafiti na wasimamizi wa sekta za kifedha,
kubadilishana mawazo kwa lengo la kukuza upatikanaji na matumizi za huduma za
kifedha Tanzania.
Katika hotuba ya ufunguzi wa
mkutano huo, Afisa Mtendaji Mkuu wa FINCA,
Tanzania, Issa Ngwegwe alisema “mifumo ya teknolojia ya kidigitali ni kichocheo
kikubwa sana katika ushirikishaji wa kifedha na pia maendeleo ya mfumo wa
kidigitali ni muhimu katika kuongeza upatikanaji wa huduma hizo.”
"Mifumo ya kidigitali ya
simu za mkononi na wakala wa kibenki ni vipengele muhimu katika kupunguza bei
ya kuwafikia mamilioni ya watanzania ambao hawana huduma za kibenki. Ushiriki
na mitandao ya simu inaonyesha fursa ya kukuza upatikanaji wa huduma za
kifedha. “ Aliongeza.
Akiongea katika mkutano huo
Mkurugenzi Mtendji wa wa FINCA Canada Bi. Stephanie Emond alisema kwamba
ushiriki wa Mastercard Foundation umeweka misingi mizuri ya ukuwaji kwa kupitia
matumizi ya teknolojia ya kifedha na mafunzo kwa lengo la kuboresha huduma na
kukuza uwezo wa FINCA pamoja na uelewa mzuri zaidi wa mahitaji ya wateja na
matokeo ya mipango ya ushirikishwaji wa fedha kwao.
“Tunaamini kwamba kupitia mkutano
huu tutajifunza kutoka safari yetu na tujenge uhusiano wa karibu miongoni mwetu
pamoja na nafasi nzuri ya kukabiliana na changamoto za soko alikadhalika na
kuweka mazingira mazuri kwa ukuwaji wa huduma za kifedha na uendeshwaji wa
sekta hiyo.” Alisema Bi. Stephanie.
Kwa upande wa mgeni rasmi Dr.
Ashatu Kijaji, Naibu waziri wa fedha na
Mipango alisisitiza kuwa serikali imekusudia kukuza ushirikishaji wa kifedha
kupitia uwekaji wa kanuni stamilifu na uratibu mzuri pamoja na mazingira mazuri
kwaajili ya ushirikishaji wa kifedha ambao utapeleka huduma za kifedha kwa watu maskini kukiwa na hatua stahiki za
kumlinda mtumiaji.
No comments:
Post a Comment