Tuesday, February 27, 2018

PICHA - IGP SIRRO AZUNGUMZA NA WANANCHI WA KAHAMA MKOANI SHINYANGA

Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akizungumza na wananchi wa Kahama mkoani Shinyanga mara alipowasili katika wilaya hiyo kwa ziara ya kikazi ya kuzungumza na maofisa na askari wa Jeshi hilo, IGP Sirro amewataka wananchi hao kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi hilo pamoja na kuwafichua wahalifu waliopo kwenye maeneo yao. Picha  na Jeshi la Polisi.

Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia mkoa wa Shinyanga, wakiimarisha ulinzi wakati Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, aliposimamisha msafara wake ili kuzungumza na wananchi waliojitokeza barabarani katika mji wa Kahama mkoani Shinyanga leo. Picha na Jeshi la Polisi.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga Simon Haule (aliyesimama) akitoa hotuba mbele ya Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, aliyewasili mkoani humo kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kuzungumza na Maofisa na askari wa Jeshi hilo na kuwakumbusha kutimiza wajibu wao wa kutenda haki kwa wananchi wanaowahudumia. Picha  na Jeshi la Polisi.

Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akiwa katika picha ya pamoja na askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia wa mkoa wa Shinyanga leo akiagananao mpakani mwa mkoa huo na wilayani Mbogwe, Geita, IGP Sirro yupo mkoni humo kwa ziara ya kikazi. Picha  na Jeshi la Polisi.


No comments: