Kampuni ya simu za mikononi ikiwa
chini ya kampuni mama ya TRANSSION HOLDINGS iliyopo China, imeachilia rasmi
simu janja “smartphone” mpya yenye kioo kamili/enea au kwa lugha ya kiingereza
(Full DISPLAY) yenye ukubwa wa uwiano “ratio” 18:9. TECNO CAMON CM ni simu mpya
kabisa kwa mwaka 2018 .
Mambo mengi
yanatarajiwa na wadau kutoka katika simu hii mpya “CAMON CM” kwani ni
muendelezo wa toleo lililopita la CAMON.
CAMON CM inabeba sifa
kuu kubwa ambayo ni kua na kioo enea/kamili “FULL DISPLAY” chenye uwiano wa
18:9, kuifanya simu hii kua ya kwanza kutoka TECNO ambayo kioo chake hakina
mipaka au mikato kulinganisha na simu zingine zenye ukubwa wa 16:9.
Pia simu ina urefu wa
nchi 5’7 ambayo itamuwezesha mtumiaji kutazama video, kucheza michezo “Games”,
kuperuzi mitandao kwa raha zaidi kulinganisha na simu ambazo zina mipaka.
Camon
CM inamonekano wa kifahari na
umbo jembamba lenye ukubwa wa 7.75 mm.
Vigezo vingine ambavyo vinapatikana kwenye CAMON
CM ni pamoja na kamera bomba yenye uwezo wa 13MP kamera ya mbele na nyuma,4G
LTE, RAM 2GB, ROM 16GB, na betri yenye ukubwa wa 3000 mAh (Isiyotoka).
Simu hii ina rangi tatu ambazo ni
“CITY BLUE”, MIDNIGHT BLACK na “CHAMPAGNE GOLD
CAMON CM sasa
inapatikana,kwa taarifa zaidi tembelea http//www.tecno-mobile.com/tz
No comments:
Post a Comment