TBL yatoa ufafanuzi juu
ya madai kudukuliwa mfumo wake wa taarifa
Yatangaza punguzo la bei ya rejareja kwa bia ya
Castle Lite Premium Lager
Kampuni
ya Bia Tanzania (TBL), leo imetoa ufafanuzi juu ya taarifa za kudukuliwa kwa
mfumo wake wa kuhifadhi taarifa na kusisitiza kuwa mfumo wako na taarifa zake
zipo salama.
Kwa siku kadhaa, kumekuwepo na taarifa kwenye vyombo mbali
mbali vya habari kuwa, mfumo wa kuhifadhi taarifa wa TBL umedukuliwa na watu
wasiojulikana na hivyo kuhatarisha kuvuja kwa taarifa zake muhimu.
Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,
Murugenzi wa Masoko wa TBL, (Afrika Mashariki), Thomas Kemphuis alisema, baada
ya uchunguzi wa kina kampuni hiyo imejiridhisha pasipo na shaka kuwa hakuna
tukio la aina hiyo lililotokea na kusisitiza taarifa zake zipo salama huku
ikiwataka wanahisa wake, wadau pamoja na umma kwa ujumla kutokuwa na wasiwasi.
“Baada ya uchunguzi wa kina wa wataalamu wetu wa ndani na nje,
TBL inapenda kuuthibitishia umma kuwa mfumo wetu wa kuhifadhi taarifa
haujadukuliwa wala kuguswa kwa namna yoyote ile. Tunapenda kuwaambia wanahisa
wetu, wadau na umma kwa ujumla wasiwe na wasiwasi kwa kuwa hakuna tukio la aina
hii,” alisema Kemphuis.
Akisisitiza nia ya TBL
kuendelea kutoa huduma bora, Kemphuis alisema kampuni hiyo inachukulia kwa
uzito mkubwa suala la usalama wa mifumo yake na ndiyo sababu ya kufanya
uchunguzi wa haraka na wakina mara baada ya kupata taarifa za uvumi juu ya
udukuzi.
“Usalama ni moja kati ya nguzo muhimu sana kwenye utendajii
wa TBL. Tunafurahi kujivunia historia nzuri ya usalama ambayo tumekuwa nayo kwa
miaka mingi,” alisema.
Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa TBL itaendelea kutengeneza
mifumo imara ya ulinzi wa taarifa zake ili kuepuka matukio yasiyotarajiwa kama
udukuzi.
Wakati huo huo, TBL imetangaza habari njema kwa wateja wake
baada ya kutoa punguzo la bei kwa bia yake pendwa ya Castle Lite Premium Lager
kutoka bei ya sasa ya shilingi elfu 2,500 hadi shilingi 2,000.
Kwa mujibu wa Kemphuis, punguzo hilo la bei ni zawadi kwa
wateja wa bia hiyo kwa kuwa wateja waaminifu na zaidi kwa kuiunga mkono kampuni
ya TBL kupitia bidhaa zake.
“Kupunguza bei ya bia ya Castle Lite Premium Lager
kunadhihirisha shukrani zetu kwa wateja wetu kwa kutuunga mkono kwa kipindi
kirefu. TBL siku zote ipo tayari kuwasikiliza wateja wake na kuwapa kile
wanachokitaka,” alibainisha.
Kemphuis pia aliongeza kwamba wanaelewa kuhusiana na
kushindwa kuleta tamasha hilo nchini ila akaeleza kuhusu utaratibu wa
kuhakikisha Wanzania wanashiriki tamasha hilo.
“Tunajiandaa kuwapeleka watanzania 12 nchini Afrika ya kusini
kuhudhuria tamasha la Castle Lite Unlocks litakalofanyika mwezi wan ne,
utaratibu zaidi utatolewa,” alisema Kemphuis.
No comments:
Post a Comment