Friday, February 23, 2018

LIGI KUU YA WANAWAKE YA SERENGETI PREMIUM LITE KUZINDULIWA RASMI NA WAZIRI MWAKYEMBE JUMAPILI

Ligi Kuu ya Wanawake ya Serengeti Premium Lite hatua ya Nane bora inataraji kuzinduliwa rasmi mkoani Kigoma Jumapili Februari 25,2018 kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika.
Tokeo la picha la ligi kuu wa wanawake
Mchezo utakaotumiwa kuzindua ligi hiyo utazikutanisha timu za Kigoma Sisterz ya Kigoma dhidi ya Simba ya Dar es Salaam.
Aidha uzinduzi utaenda sanjari na mpango maalumu wa FIFA wa kuhamasisha soka la Wanawake uliopewa jina la Live Your Goal ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dr.Harrison Mwakyembe.
Mbali na mechi ya uzinduzi mechi nyingine za ligi hiyo ya Wanawake ya Serengeti Premium Lite zinatarajia kuchezwa kesho kwenye viwanja tofauti.
Uwanja wa Samora Panama FC watacheza dhidi ya Evergreen Queens ya Dar es Salaam saa 10 jioni,huko Mbweni JKT Queens watacheza dhidi ya Alliance saa 10 jioni,mabingwa watetezi Mlandizi Queens wanasafiri mpaka Jamhuri Dodoma kucheza na Baobab Queens.

Wakati huohuo Kozi ya makocha wa kozi ya grassroots kwa watoto wenye umri wa miaka 6-12 Wasichana na Wavulana imeanza Jumatano kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika,Ujiji,Kigoma.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA TFF

No comments: