Daktari wa kwanza mwanamke nchi Tanzania Ester Mwaikambo akizindua progaram hiyo mapema leo makao makuu ya Mtandao wa Jinsia(TGNP) yaliyopo mabibo jijini Dar es salaam. |
Programu hiyo
iliyopewa jina la “Mentorship Program” itawasaidia watoto wa kike kuweza kusimama
wenyewe katika nafasi za uongozi na maamuzi kwa kupewa elimu na watu
waliowatangulia katika nafasi hizo au
kwa jina lingine makungwi watakao walea na kuwaonyesha njia na mbinu za kuwa
kama wao.
Akiongea na
waandishi wa habari katika uzinduzi wa programu hiyo leo jijini Dar es salaam Mratibu
wa Mafunzo ya Jinsia Jane Tesha alisema kuwa lengo kuu la programu hiyo ni kuwalea vijana wakike walio
katika uongozi au wanaotarajiwa kuingia katika uongozi ili waweze kuwa imara
katika nafasi zao.
Aliongeza
kwa kusema kuwa jumla ya washiriki 33 watapata nafasi ya kukuzwa na kufunzwa
jinsi ya kuzitumia rasilimali walizonazo kupitia makungwi walioteuliwa
kuwafunza katika nyanja tofauti tofauti.
Aidha Dada
Jeni aliendelea kusema kuwa mafunzo hayo yatakuwa ya miezi 6 na washiriki
watapewa mafunzo katika Nyanja kama afya, uandisi, wanasheria, biashara na
nyingine nyingi ili kuendelea kuongeza pato la taifa kupitia vijana ambao ni asilimia
61 ya watanzania wote.
“Elimu hii
tutakayoitoa kwa wanawake hasa vijana ambao ni asilimia 61 ya watanzania wote,
itawasaidia kujitambua na kutambua fursa mbalimbali walizonazo na kuwa na
ujasiri wa kugombea pamoja na kushiriki katika nafasi mbalimbali za uongozi na
maamuzi ili kuweza kufikia malengo ambayo 50 kwa 50 katika uongozi kati ya
wanawake na wanaume”. Alisema Dada Jeni
Kwa upande
wake Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao Lilian Liundi alisema huu ni mwanzo tu
tumeanza na vijana wa mjini kwa kuwapa fursa hii lakini tunaandaa mpango
mwingine ambao utakuja hivi karibuni ambao utawagusa na wale wa vijijini.
Baadhi ya Waandishi wa habari pamoja wageni mbalimbali waliofika kushuhudia uzinduzi huo wakifuatilia kwa umakini matukio yanayoendelea katika uzinduzi huo. |
“Kwa
wasichana ambao wapo vijijini na hawana chanzo chochote cha mtandao hawa ndio
malengo yetu makuu, hivyo basi tutahakikisha wanapata elimu hii kwa kuwapelekea
makungwi waweze kuwapika kupitia vituo vyetu vya taarifa na maarifa ili
wasiweze kupitwa na programu hii”. Alisema Mkurugenzi
ANGALIA VIDEO HII KUJIONEA UZINDUZI HUO...
No comments:
Post a Comment